Home
All posts
Friday, April 3, 2020
Wednesday, April 1, 2020
MAJALIWA: ATAKAYETHIBITIKA NA CORONA APELEKWE ENEO MAALUMU BILA KUJALI CHEO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesisitiza kuwa mtu yeyote akithibitika kuwa na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) apelekwe eneo maalum bila kujali cheo chake na atalala palipoandaliwa.
Amewataka Watanzania wazingatie masharti ya afya kwa kufuata ushauri unaotolewa na Serikali kwa sababu hivi sasa nchi yetu na dunia kwa ujumla inapitia katika kipindi kigumu pia,waendelee kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha
Bungeni hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na
Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.
AmesemaMachi 11, 2020, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ijulikanayo kama COVID-19inayosababishwa
na virusi vya CORONA kuwa ni janga la Kimataifa. Aidha, tarehe 16
Machi, 2020 Serikali ilitangaza kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza nchini, ni
muhimu wananchi kuchukua tahadhari.
Waziri Mkuu amesema tangu kugundulika kwa ugonjwa huo, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi, upimaji na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini.
Amesema la hatua hizo ni kuwabaini wasafiri wanaoonesha dalili za ugonjwa wa COVID-19 au wenye viashiria hatari, hata hivyo mashirika mengi yamesitisha ndege zao kwa kukosa abiria. “Abiria wote waingiao nchini hupelekwa Isolation house.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema katika kukabiliana na virusi vya corona, Serikali ilitoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo kusitisha Mbio za Mwenge wa Uhuru na fedha zilizotengwa kwa ajili ya jukumu hilo zitumike kusaidia hatua za kukabiliana na janga hilo.
“Mbali na kusitidsha mbio za mwenge Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo ligi kuu ya Tanzania Bara, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili na aina nyingine za michezo.”
Amesema
Serikali pia imesitisha shughuli zote za elimu kuanzia elimu ya awali,
msingi, sekondari, vyuo vya kati hadi vyuo vikuu pamoja na semina,
warsha, makongamano na mikutano yote ya ndani na ya hadhara yenye
kuhusisha mjumuiko wa watu wengi.
Amesema
suala lingine ni kuwatenga abiria waingiao nchini kwenye maeneo maalum
kwa siku 14 ili kufuatilia hali zao mpaka tutakapojiridhisha kuwa hana
ugonjwa ili kuhakikisha maambukizi ya virusi hivyo hayasambai kwa jamii.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Serikali inawasisitiza Watanzania kufuata kanuni za
kudhibiti maambukizi ikiwemo kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na
sabuni, kukinga unapokohoa na kupiga chafya, kutopeana mikono, kukaa au
kusimama kwa umbali na jirani yako.
Pia,
Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuwaasa Watanzania wenye safari
zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi ya virusi vya Corona,
kusitisha safari hizo, na hatua zingine zitafuata.
Amesema
Serikali inaendelea na usimamizi wa karibu sambamba na kufanya tathmini
na kuchukua hatua kadhaa. “Tumeunda Kamati za kitaifa tatu
zinazosimamia ugonjwa huu, niendelee kusisitiza kuwa sote tuzingatie
maelekezo yaliyotolewa na Serikali toka tulipoanza kampeni ya kupambana
na ugonjwa huu.”
Wakati huo huo, Wazirti Mkuuamesema
Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba liidhinishe
jumla ya sh. 312,802,520,000; kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo.
Vilevile
Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh. 121,786,257,000
kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, sh. 113,567,647,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo.
(MWISHO)
VIJIJI 9,001 NCHINI VIMEUNGANISHIWA UMEME -MAJALIWA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kutekeleza Mradi wa
Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) ambapo vijiji vilivyounganishiwa
umeme nchini vimeongezeka kutoka vijiji 2,118 mwaka 2015 hadi vijiji
9,001 mwezi Machi 2020.
Amesema kuwa jumla yataasisi
11,128 zikiwemo za elimu, afya, dini, mashine za kusukuma maji na
huduma za biashara zimenufaika na mradi, hivyo mafanikio hayo pamoja na
mengine makubwa yaliyopatikandani ya kipindi cha takriban miaka mitano yamesaidia kuimarisha hali ya kiuchumi wa Taifa na kijamii kwa ujumla.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha Bungeni
hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge
kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.
“Mheshimiwa Spika,tarehe
20 Novemba 2015 wakati akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli aliwaahidi wananchi wote kuwa Serikali ya Awamu ya Tano
itawatumikia na kuwajali.
Waziri
Mkuu amesema katika kutekeleza azma hiyo, ujenzi wa miundombinu muhimu
ya kiuchumi hususan ya usafiri na usafirishaji sambamba na uimarishaji
wa huduma muhimu za kijamii ni miongoni mwa masuala yaliyopewa
kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesema
ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, ufufuaji wa Shirika
la Ndege la Tanzania na urejeshwaji wa mali za ushirika mfano, NCU,
SHIRECU ni kati ya hatua za msingi zinazochukuliwa na Serikali katika
kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na sekta ya viwanda ifikapo 2025.
Waziri
Mkuu amesema hatua nyingine ni pamoja na urejeshwaji wa mali za Mamlaka
ya Mkonge Tanzania, ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere,
ulinzi wa maliasili na rasilimali za Taifa pamoja na ujenzi na ukarabati
wa miundombinu ya Elimu, Afya na Maji.
“Katika
kipindi hiki cha miaka mitano, tumeshuhudia miradi hiyo muhimu ikiwa
katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kwa mfano, ujenzi wa Reli ya
Kati kwa kiwango cha Kimataifa ambao hadi Machi 2020 umetumia sh.
trilioni 2.96 na kukamilika kwa asilimia 75 kwa kipande cha Dar es
Salaam hadi Morogoro na asilimia 28 kwa kipande cha Morogoro hadi
Makutupora.”
Amesema
utekelezaji wa mradi huo umewezesha utoaji wa zabuni zenye thamani ya
sh. bilioni 664.7 kwa wazabuni na wakandarasi wa ndani 640, ajira
zipatazo 13,177 za kitaalam na zisizo za kitalaam zimezalishwa na kati
ya hizo, ajira za kitaalam kwa wazawa ni asilimia 46.5 ikilinganishwa na
asilimia 53.5 ya wageni.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Serikali inatumia gharama kubwa katika kujenga
miundombinu hiyo wezeshi ya kiuchumi kwa lengo la kulifanya Taifa kuwa
na uchumi imara wa kujitegemea na wenye kuhimili ushindani. Fedha hizo
pia zimekuwa chanzo cha ajira na zabuni kwa Watanzania zinazowasaidia
kuongeza kipato.
“Mradi
huu utakapokamilika utaongeza ufanisi wa huduma za usafiri na
usafirishaji wa bidhaa na abiria pamoja na kupunguza gharama za uchukuzi
pia utachochea ukuaji wa miji na sekta nyingine kama vile kilimo,
viwanda, utalii na biashara. Vilevile, mradi huu utakuwa chanzo cha
ongezeko la mapato ya Serikali yatakayosaidia katika kuboresha maslahi
ya watumishi na huduma za kijamii kama vile afya, elimu na maji.”
Vilevile,
Waziri Mkuu amesema ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji wa
Julius Nyerere linalotarajiwa kuzalisha Megawati 2,115, hadi Machi 2020
mradi huo umegharimu sh. trilioni 1.28 na umekamilika kwa asilimia
10.74.
Amesema
kukamilika kwa bwawa hilo kutalihakikishia Taifa letu umeme wa uhakika
na wa nafuu zaidi. Aidha, ongezeko hilo la uzalishaji wa umeme
litawezesha shughuli za uzalishaji viwandani kuwa za uhakika, tija,
ufanisi na gharama nafuu zaidi. “Vilevile, mradi huu utachangia kwa
kiasi kikubwa katika juhudi za kuhifadhi mazingira kutokana na
kuongezeka kwa matumizi ya nishati ya umeme badala ya kuni.”
Hata
hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa kila mwananchi kuendelea kuunga
mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi
chini ya uongozi mahiri na thabiti wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu, tija na ufanisi, uaminifu na
kupiga vita rushwa.
Wakati huo huo, Wazirti Mkuuamesema
Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba liidhinishe
jumla ya sh. 312,802,520,000; kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo.
Vilevile
Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh. 121,786,257,000
kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, sh. 113,567,647,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo.
WAZIRI MKUU ATOA NENO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu ni vema viongozi
wa vyama vya siasa nchini wakaonesha mfano wa kuendesha siasa za
kistaarabu zenye lengo la kuwaunganisha watanzania na siyo
kuwatenganisha.
“Hivyo
basi, tudumishe utulivu, amani, mshikamano pamoja na ustaarabu wetu wa
Kitanzania katika kipindi chote cha kampeni na Uchaguzi Mkuu ili
kulifanya Taifa letu kuendelea kuwa kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa
barani Afrika na duniani kwa ujumla.”
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha Bungeni
hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge
kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.
Pia, Waziri Mkuu amewasihi
Watanzania washiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kwa kufuata
sheria, kanuni na taratibu za Nchi. “Hakuna kiongozi aliyewahi kupata
sifa nzuri kwa kuwa chanzo cha mifarakano.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga
kura kwa awamu ya pili linatarajiwa kuanza Aprili 5, 2020 na kukamilika
Juni 26 2020.
“Zoezi
hili litaenda sambamba na uhakiki wa taarifa za wapiga kura katika
daftari hilo. Natoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha
na kuboresha taarifa zao katika daftari hilo, ili waweze kutumia haki
yao ya Kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.”
Waziri Mkuu amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2020 nchini.
Amesema
pamoja na mambo mengine, maandalizi hayo yanahusisha Zoezi la Kuboresha
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika nchi nzima. Awamu ya
kwanzailizinduliwa tarehe 18 Julai, 2019 Mkoani Kilimanjaro na kukamilika tarehe 23 Februari, 2020 katika Mkoa wa Dar es Salaam.
“Uboreshaji
wa daftari hili ulihusisha uandikishaji wa wapiga kura wapya ambao
wametimiza umri wa miaka 18 au watatimiza umri huo ifikapo siku ya
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; urekebishaji wa taarifa za wapiga kura
walioandikishwa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na ufutaji wa taarifa
za Wapiga Kura waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura.”
Amesema katika zoezi hilo, jumla ya wapiga
kura 10,285,732 wameandikishwa na kati yao, wapiga kura wapya ni
7,043,247, walioboreshewa taarifa zao ni 3,225,778 na wapiga kura
waliofutwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutokana na kupoteza
sifa ni 16,707.
Wakati huo huo, Wazirti Mkuuamesema
Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba liidhinishe
jumla ya sh. 312,802,520,000; kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo.
Vilevile
Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh. 121,786,257,000
kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, sh. 113,567,647,000 ni
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo.
SERIKALI YAWEZESHA UPATIKANAJI AJIRA MILIONI 12.6
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
utekelezaji wa miradi ya maendeleo na
uboreshaji wa huduma za jamii unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano
umechangia kuzalisha ajira milioni 12.6
kwenye sekta mbalimbali nchini.
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Aprili mosi, 2019) wakati akiwasilisha hotuba kuhusu
Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021.
“Mafanikio haya katika utekelezaji wa miradi ya
maendeleo na uboreshaji wa huduma za jamii yameenda sambamba na uzalishaji wa
ajira zipatazo milioni 12.6 zikiwemo ajira za moja kwa moja milioni 11.7 kwenye
sekta mbalimbali nchini,” amesema.
Akitoa mfano Waziri Mkuu amesema sekta za afya, elimu na utawala zimetoa
ajira za kudumu kwa kuajiri watumishi 28,403 katika mamlaka za Serikali za
Mitaa; ufufuaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) pamoja na kuboresha
viwanja vya ndege umetoa jumla ya ajira 2,970 huku ujenzi wa viwanda
nchini ukichangia ajira 41,900.
“Mradi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa umewezesha kuzalishwa
ajira zipatazo 13,177 za kitaalam na zisizo za kitalaam. Kati ya hizo,
ajira za kitaalam kwa wazawa ni asilimia 46.5. Pia, kupitia mradi huu kumekuwa
na utoaji wa zabuni zenye thamani ya shilingi bilioni 664.7 kwa wazabuni na
wakandarasi wa ndani 640,” ameongeza.
“Mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere kupitia maporomoko ya mto Rufiji
umezalisha jumla ya ajira 3,897 ikiwemo ajira za wazawa 3,422.”
Amesema jumla ya mafundi 845,348 walipata ajira za mikataba na
muda kwenye ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Hospitali za
Wilaya, vituo vya afya, zahanati, madarasa, nyumba na majengo maeneo mapya ya
utawala, miradi ya barabara chini ya TARURA kwa kutumia Force Account.
Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu amesema Serikali ya
Awamu ya Tano imefanikiwa katika usimamizi madhubuti wa sheria, kanuni na
taratibu za uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma. “Usimamizi huo,
umewezesha viongozi na watendaji wa umma kuwajibika ipasavyo kwa wananchi ambao
ndiyo waajiri wao. Sambamba na hilo, nidhamu Serikalini imeongezeka kutokana na
Serikali kuwachukulia hatua za kinidhamu
watumishi wazembe, wadanganyifu na wasio waadilifu.”
Waziri Mkuu amesema mafanikio yote hayo yanachangiwa na uongozi mahiri wa
Rais Dkt. John Pombe Magufuli. “Tunapotaja mafanikio haya tuna kila sababu ya
kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwani uongozi wake mahiri na wenye uthubutu ndiyo msingi
mkuu wa mafanikio yaliyopatikana.”
“Dhana
na falsafa aliyojenga ya Hapa Kazi Tu imesaidia kubadili mtazamo wa
Watanzania wengi ambapo sasa tunashuhudia uwajibikaji wa kiwango cha juu wa mtu
mmoja mmoja, katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na uzalishaji iwe shambani,
ofisini, kiwandani, sokoni na kwingineko badala ya tabia ya awali ya baadhi ya
wananchi wachache kupoteza muda mwingi katika shughuli zisizokuwa na tija kwa
Taifa.”
(mwisho)
WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, ASOMA HOTUBA YA MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI, PAMOJA NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA 2020/2021
| Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ikiwaambia Wabunge wazingatie matumizi ya senitizer, katika kujikinga na ugonjwa wa Corona, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 1, 2020. |
Sunday, March 29, 2020
MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU WA ZANZIBAR
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu, Brigedia Jenerali Mstaafu, Ramadhani Haji Faki yaliyofanyika Mkwajuni Zanzibar, Machi 29, 2020. |
MAJALIWA ATOA POLE KWA FAMILIA YA SOKOINE
Thursday, March 26, 2020
MAJALIWA: KAMATI ZA MAAFA ZIUNGANE NA WARATIBU WA KUKABILIANA NA CORONA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za Maafa katika ngazi za mikoa na wilaya ziungane na waratibu wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) waliopo katika maeneo yao.
Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza Watanzania waendelee kujikinga na ugonjwa huo kwa kuhakikisha wanajiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na hata wakienda kwenye maeneo ya kutolea huduma kama sokoni, vituo vya mabasi wapeane nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 26, 2020) wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Kitaifa cha Kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma. Kikao hicho kimehusisha wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipeleke wataalamu katika maeneo yenye mahitaji makubwa kama kwenye viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandarini.
“Lengo letu ni kuhakikisha nchi inabaki salama hivyo Watanzania tuendelee kuwa na tahadhari ya kutosambaa kwa ugonjwa huu na pale tunapokwenda kwenye maeneo ya kutolea huduma tujipe nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.”
Waziri Mkuu amesema kamati hiyo inatakiwa ifuatilie na isimamie vizuri ili kuhakikisha watu wote wanaoingia nchini wanapimwa na wanafuatilia ili kujua historia zao za safari katika kipindi cha siku 14, lengo likiwa ni kuzuia maambukizi hayo yasisambae kwa jamii.
Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuratibu zoezi la kupeleka watu walioko kwenye karantini, wahakikishe wahusika wanafika kwenye hoteli walizozichagua. Pia Serikali inafanya utaratibu wa kutenga maeneo ambayo watu watakuwa wanakaa bila gharama na yatakuwa na huduma zote muhimu.
Pia, Waziri Mkuu amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya corona, ambapo amevitaka viendelee na utaratibu huo kwani utasaidia wananchi kupata elimu na kuweza kujikinga na maabukizi hayo.
Machi 23, 2020, Waziri Mkuu aliunda kamati tatu kwa ajili ya kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi ya corona (COVID-19).
Kamati hizo ni ya Kitaifa ambayo inaongozwa na Waziri Mkuu na itahusisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Wengine ni Waziri Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Pia, Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Msemaji Mkuu wa Serikali, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katika kikao cha leo, Waziri Mkuu ameongeza wajumbe wawili ili waongeze nguvu katika kukabiliana na virusi vua corona ambao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
(mwisho)
MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA KUKABILIANA NA CORONA
Tuesday, March 24, 2020
MAJALIWA AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU KUHUSU CORONA
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. |
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
-
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia sukari, alipotembelea kiwanda cha Kilombero Sugar, kilichopo katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Mo...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati ina...
-
*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya sik...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo ya namna mashine zinavyochakata mifuko chakavu na ...
-
Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu H...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.