WAZIRI
 MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kutekeleza Mradi wa 
Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) ambapo vijiji vilivyounganishiwa 
umeme nchini vimeongezeka kutoka vijiji 2,118 mwaka 2015 hadi vijiji 
9,001 mwezi Machi 2020. 
Amesema kuwa jumla yataasisi
 11,128 zikiwemo za elimu, afya, dini, mashine za kusukuma maji na 
huduma za biashara zimenufaika na mradi, hivyo mafanikio hayo pamoja na 
mengine makubwa yaliyopatikandani ya kipindi cha takriban miaka mitano yamesaidia kuimarisha hali ya kiuchumi wa Taifa na kijamii kwa ujumla.
Waziri
 Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 1, 2020) akiwasilisha Bungeni
 hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya 
Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge 
kwa mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma.
“Mheshimiwa Spika,tarehe
 20 Novemba 2015 wakati akifungua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe 
Magufuli aliwaahidi wananchi wote kuwa Serikali ya Awamu ya Tano 
itawatumikia na kuwajali.
Waziri
 Mkuu amesema katika kutekeleza azma hiyo, ujenzi wa miundombinu muhimu 
ya kiuchumi hususan ya usafiri na usafirishaji sambamba na uimarishaji 
wa huduma muhimu za kijamii ni miongoni mwa masuala yaliyopewa 
kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano.
Amesema
 ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, ufufuaji wa Shirika 
la Ndege la Tanzania na urejeshwaji wa mali za ushirika mfano, NCU, 
SHIRECU ni kati ya hatua za msingi zinazochukuliwa na Serikali katika 
kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na sekta ya viwanda ifikapo 2025.
Waziri
 Mkuu amesema hatua nyingine ni pamoja na urejeshwaji wa mali za Mamlaka
 ya Mkonge Tanzania, ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, 
ulinzi wa maliasili na rasilimali za Taifa pamoja na ujenzi na ukarabati
 wa miundombinu ya Elimu, Afya na Maji.
“Katika
 kipindi hiki cha miaka mitano, tumeshuhudia miradi hiyo muhimu ikiwa 
katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kwa mfano, ujenzi wa Reli ya 
Kati kwa kiwango cha Kimataifa ambao hadi Machi 2020 umetumia sh. 
trilioni 2.96 na kukamilika kwa asilimia 75 kwa kipande cha Dar es 
Salaam hadi Morogoro na asilimia 28 kwa kipande cha Morogoro hadi 
Makutupora.”
Amesema
 utekelezaji wa mradi huo umewezesha utoaji wa zabuni zenye thamani ya 
sh. bilioni 664.7 kwa wazabuni na wakandarasi wa ndani 640, ajira 
zipatazo 13,177 za kitaalam na zisizo za kitalaam zimezalishwa na kati 
ya hizo, ajira za kitaalam kwa wazawa ni asilimia 46.5 ikilinganishwa na
 asilimia 53.5 ya wageni.
Kadhalika,
 Waziri Mkuu amesema Serikali inatumia gharama kubwa katika kujenga 
miundombinu hiyo wezeshi ya kiuchumi kwa lengo la kulifanya Taifa kuwa 
na uchumi imara wa kujitegemea na wenye kuhimili ushindani. Fedha hizo 
pia zimekuwa chanzo cha ajira na zabuni kwa Watanzania zinazowasaidia 
kuongeza kipato.
“Mradi
 huu utakapokamilika utaongeza ufanisi wa huduma za usafiri na 
usafirishaji wa bidhaa na abiria pamoja na kupunguza gharama za uchukuzi
 pia utachochea ukuaji wa miji na sekta nyingine kama vile kilimo, 
viwanda, utalii na biashara. Vilevile, mradi huu utakuwa chanzo cha 
ongezeko la mapato ya Serikali yatakayosaidia katika kuboresha maslahi 
ya watumishi na huduma za kijamii kama vile afya, elimu na maji.”
Vilevile,
 Waziri Mkuu amesema ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji wa 
Julius Nyerere linalotarajiwa kuzalisha Megawati 2,115, hadi Machi 2020 
mradi huo umegharimu sh. trilioni 1.28 na umekamilika kwa asilimia 
10.74. 
Amesema
 kukamilika kwa bwawa hilo kutalihakikishia Taifa letu umeme wa uhakika 
na wa nafuu zaidi. Aidha, ongezeko hilo la uzalishaji wa umeme 
litawezesha shughuli za uzalishaji viwandani kuwa za uhakika, tija, 
ufanisi na gharama nafuu zaidi. “Vilevile, mradi huu utachangia kwa 
kiasi kikubwa katika juhudi za kuhifadhi mazingira kutokana na 
kuongezeka kwa matumizi ya nishati ya umeme badala ya kuni.”
Hata
 hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa kila mwananchi kuendelea kuunga 
mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi 
chini ya uongozi mahiri na thabiti wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa 
kufanya kazi kwa bidii, weledi, uadilifu, tija na ufanisi, uaminifu na 
kupiga vita rushwa.
Wakati huo huo, Wazirti Mkuuamesema
 Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini yake inaliomba liidhinishe
 jumla ya sh. 312,802,520,000; kati ya fedha hizo, sh. 88,429,156,000 ni
 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 224,373,364,000 ni kwa ajili ya
 matumizi ya maendeleo.
Vilevile
 Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe jumla ya sh. 121,786,257,000 
kwa ajili ya Mfuko wa Bunge. Kati ya fedha hizo, sh. 113,567,647,000 ni 
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,218,610,000 ni kwa ajili ya 
matumizi ya maendeleo.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.