Wednesday, November 15, 2017

KILIMO WATAKIWA KUTAFITI MBEGU BORA ZA PAMBA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo ifanye utafiti wa kina ili kupata aina bora ya mbegu za pamba zitakazowanufaisha wakulima.

Amesema ni lazima utafiti huo ufanyike kwa kuzingatia aina ya udongo unaopatikana katika kila mkoa unaolima pamba.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Novemba 14, 2017) alipozungumza na wabunge wanaotoka katika mikoa inayolima pamba, Bungeni mjini Dodoma.

“Mbegu za pamba ziko nyingi na zina migogoro. Mbegu nyingine zina manyoya, nyingine zina vipara hivyo lazima utafiti wa kina ufanyike ili kupata aina bora.”

Alisema Wizara ya Kilimo itumie taasisi zake vikiwemo vyuo kufanya uchunguzi na kubaini ni aina gani za mbegu zinafaa kutumika kulingana na eneo husika.

Alisema utafiti huo ambao utabainisha aina ya mbegu inayofaa kulingana na aina ya udongo katika kila eneo ili kumuwezesha mkulima kupata mazao ya kutosha.

Pia aliwataka Maofisa Kilimo katika mikoa inayolima mazao makuu ya biashara waweke kipaumbele katika kuyasimia mazao hayo.

Waziri Mkuu alisema Maofisa hao lazima wahakikishe wanayasimamia vizuri mazao hayo ambayo ni korosho, chai, pamba, kahawa na tumbaku ili yawe na tija.

Alisema Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemo na zao la pamba.

Waziri Mkuu alisema Serikali inataka kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba, pembejeo hadi masoko.

“Tunataka kulifanya zao hilo ambalo lilikuwa likijulikana kama dhahabu nyeupe lifikie kiwango cha juu cha uzalishaji, hivyo kuongeza tija kwa wakulima.”

Pia Waziri Mkuu aliwaagiza Maofisa Kilimo katika mikoa hiyo wafanye sensa ili kutambua idadi ya wakulima wa pamba na ukubwa wa mashamba yao.

Alisema lengo la sensa hiyo ni kutambua idadi ya wakulima na ukubwa wa mashamba yao ili kurahisisha usambazaji wa pembejeo kulingana na mahitaji.

Wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wabunge waliiomba Serikali kuhakikisha zao hilo linaboreshwa ikiwa ni pamoja na kuwafikishia wakulima pembejeo kwa wakati.

Kwa upande wake Mbunge wa Itilima Bw. Njalu Silanga aliiomba Serikali izibane Halmashauri ili kuhakikisha fedha za miradi ya kilimo zinatumika ipasavyo.

Bw. Silanga alisema msukumo wa Serikali wa kufufua zao la pamba umeanza kuzaa matunda, hivyo aliiomba Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kutafuta masoko ya kutosha.

Naye Mbunge wa Tarime Mjini, Bi Ester Matiko ameiomba Serikali kuwaelimisha wananchi na kuwahamasisha kulima kilimo hicho ili waachane na kilimo cha bangi.

“Serikali ikitilia mkazo katika usimamizi wa mazao hayo tutasonga mbele na Tanzania ya viwanda tutaiona. Wakulima waelimishwe kuwa mazao hayo yana tija, hivyo wataachana na kilimo cha bangi.”

Bi. Ester alisema kati ya mazao makuu matano ya biashara manne yanalimwa katika jimbo lake ambayo ni chai, pamba, kahawa na tumbaku, hivyo wakulima wakipewa elimu ya kutosha juu za mazao hayo watapata tija.

Read More

KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR YAVUTIWA NA URATIBU WA AFYA MOJA TANZANIA BARA

Kamisheni ya Kukabiliana na maafa Zanzibar imevutiwa na shughuli za kuratibu maafa nchini zinazofanywa na serikali ya awam ya Tano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Idara ya Kuratibu maafa ikiwa ni pamoja na kuratibu Afya moja ambapo katika Dhana ya Afya Moja, sekta ya   afya ya binadamu, wanyama (pori na wafugwao) na mazingira, zinakuwa na mawasiliano ya karibu kiutendaji na kupanga  mikakati ya pamoja katika kujiandaa na milipuko ya magonjwa na kukabiliana nayo endapo itatokea.

Akiongea wakati wa  ziara ya Kubadilishana Uzoefu na Idara ya Kuratibu Maafa na Ofisi ya Waziri Mkuu,jijini Dar es salaam leo tarehe 15 Novemba 2017, Mkurugenzi Mtendaji Kamishseni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Shaban Mohamedi amebainisha kuwa kamisheni yake imevutiwa na jinsi idara ya maafa inavyoweza  kuimarisha juhudi na ushirikiano wa sekta mbalimbali katika maandalizi ya kuzuia,kujiandaa na kukabili  magonjwa ambukizi kwa kujumuisha sekta zote muhimu.

“Tutaupitia mpango mkakati wa Afya moja  ili nasisi tuanze juhudi za kuratibu Afya moja  kwani  Kamisheni inajukumu lakukabiliana na Maafa hivyo tutachukua juhudi za kuhakikisha na sisi Zanzibar tunashirikiana na wadau husika ili tuweze kutumia rasilimali ndogotulizonazo kuweza kukabili  magonjwa yatokayo kwa  wanyama kwenda kwa binadamu yanayoiathiri jamii ya Zanzibar” alisisitiza Khatibu

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya , alifafanua kuwa suala la Afya moja linaratibiwa na ofisi yake kupitia Dawati maalum kutokana na kuwa magonjwa ya mlipuko ni masuala mtambuka na yanahitaji rasilimali watu na fedha nyingi hivyo kwa uratibu wa pamoja inasaidia kuhakikisha sekta zote zinashirikiana kukabiliana na athari za magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

“Umuhimu huu wa Afya moja unatokana na ukweli kwamba magonjwa na athari nyingine za binadamu kwa kiasi cha asilimia 60 hadi 80 huusisha wanyama. Kwa kufanya hivi ufanisi huongezeka kwani mchanganyiko wa Wataalamu, wakifanya kazi kwa pamoja na ushirikianao mkubwa, huchukua muda mfupi, na matumizi ya raslimali chache kwa pamoja huleta matokeo mazuri zaidi” Alisema Msuya.

Mwaka 2013, aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya nne, ya Jamhuriya MuunganowaTanzania, Dk. Ghalib Bilal alizindua mtandao wa afya moja jijini Arusha. Kufuatia uzinduzi huo, mwaka 2015 wadau kutoka sekta mbalimbali walikaa na kutengeneza mpango mkakati wa afya wa miaka mitano (2015 – 2020). Mpango huo umeainisha masuala yahusuyo afya moja, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa utaratibu wa kuratibu shughuli zote za afya moja katika idara ya kuratibu maafa katika ofisi ya waziri mkuu.
Read More

KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR YAVUTIWA NA URATIBU WA AFYA MOJA TANZANIA BARA

Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,Brigedia Jenerali Mbazi Msuya (Kulia), Mkurugenzi mtendaji  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  Zanzibar (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Operesheni na Huduma za Binadamu Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  Zanzibar, Makame Khatib wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya  Kamisheni hiyo na Idara ya maafa  walipofanya ziara ofisi ya Waziri Mkuu, leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.
Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu , Edgar Senga akiwasilisha mada ya majukumu ya idara hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akifafanua jambo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na  Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ya Zanzibar walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam, wengine ni waratibu wa maafa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.
Mkuu wa Kitengo cha Operesheni na Huduma za Binadamu Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa  Zanzibar, Makame Khatib akiwasilisha mada ya majukumu ya Kamisheni hiyo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu na  Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, walipofanya ziara ofisini hapo leo tarehe 15 Novemba, 2017,jijini Dar es Salaam.


Read More

SERIKALI KUZINDUA RIPOTI YA UTAFITI WA KITAIFA WA MATOKEO YA UKIMWI 2016/17

Serikali inatarajia kuzindua Ripoti ya Utafiti wa Kitaifa wa Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/2017 katika Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Desemba Mosi mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Siku ya Maadhimisho ya UKIMWI Duniani.

“Hii ni ripoti muhimu sana inayotokana na utafiti ambao huwa unafanyika kila baada ya miaka minne, ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004 ni taarifa ambayo husaidia kuonesha hali halisi ya maambukizi ya VVU kwa watu wa marika mbalimbali pamoja na mapendekezo ya kisera namipango ya kudhibiti UKIMWI nchini,” amesema Mhe. Mhagama.

Aidha, amesema kuwa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yenye kaulimbiu  “Changia mfuko wa maisha, Tanzania bila Ukimwi inawezekana”  yatatoa fursa ya kutathimini hali halisi na mwelekeo wa udhibiti UKIMWI Kitaifa na Kimataifa ikiwemo kutafakari changamoto, mafanikio na uimarishaji wa mikakati mbalimbali ya kudhibiti UKIMWI.

” Siku hii pia hutoa nafasi ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha yao kutokana na UKIMWI, kuwaenzi wale waliojitokeza na kutoa mchango wao katika kudhibiti UKIMWI, pamoja na kuwajali yatima waliotokana na vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa UKIMWI” ameongeza Jenista Mhagama.

Pia amesema kuwa, lengo lingine ni kutafakari na kutekeleza kitaifa na kimataifa kauli mbiu inayotolewa kila mwaka kulingana na vipaumbele vya kidunia, kikanda na kitaifa.

Aidha, Mhe. Mhagama amebainisha baadhi ya matukio makuu yatakayoambata katika maadhimisho hayo ni Kongamano la Kitaifa la kutathimini hali na mwelekeo wa udhibiti UKIMWI nchini litakalofanyika kati ya tarehe 28 hadi 29 Novemba mwaka huu jijini Dar es Salaam ambalo litajadili mawasiliano ya utekelezaji wa afua za ukimwi nchini ili kujua mahali tulipotoka, tulipo na tunakoelekea.

Vilevile amesema kuwa, katika maadhimisho hayo kutakuwa na uzinduzi wa Mkakati/ Mwongozo wa Taifa wa Afua za Matumizi ya kujikinga na VVU ambao utafanyika tarehe 27 mwezi huu.

“Katika Maadhimisho hayo kutakuwepo na maonesho ya shughuli za wadau wa udhibiti UKIMWI nchini yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 24 Novemba mwaka huu yakijumiisha huduma mbalimbali  na utoaji elimu na burudani kwa wananchi ikiwemo huduma za upimaji wa hiari wa VVU na ushauri nasaha, upimaji wa shingo ya kizazi, sukari, uzito, damu na elimu kupitia vikundi vya sanaa na burudani” amefafanua Mhe. Mhagama.

Mbali na hayo, Jenista Mhagama amesema kuwa, katika maadhimisho hayo Serikali itafaya uhamasishaji wa Mfuko wa Fedha za Kudhibiti Ukimwi nchini kupitia matembezi ya hisani tarehe 25 Novemba na pia chakula cha jioni maalumu kwa kuchangia mfuko huo Desemba Mosi.

Hata hivyo, Waziri Jenista ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo ili kupata huduma mbalimbali zitakazotolewa ikiwemo upimaji wa hiari wa VVU na ushauri nasaha. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amewahamasisha wananchi na wadau mbalimbali   kuchangia Mfuko wa kudhibiti Ukimwi kwa kushiriki Marathoni, kuchangia kupitia kununua tshirt kwa shilingi 20,000 na pia kuchangia kwa hiari kupitia namba 0684 909090.
Read More

SERIKALI KUZINDUA RIPOTI YA UTAFITI WA KITAIFA WA MATOKEO YA UKIMWI 2016/17

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa Habari Mjini Dodoma mapema leo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Desemba mosi mwaka huu Jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya  Kudhibiti UKIMWI TACAIDS  Dkt. Leonard Maboko.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya  Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS)  Dkt. Leonard Maboko akieleza  kwa waandishi wa Habari kuhusu shughuli  mbalimbali zitakazofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Desemba mosi mwaka huu .kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama .
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika mjini Dodoma uliofanyika Novemba 15, 2017.



Read More

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKISALIMIANA NA WATU MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA BUNGE DODOMA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mpiga Picha mwandamizi wa TBC Bibi Mary Hondo  katika Viwanja vya Bunge  Dodoma leo Novemba 15/2017 .pembeni kwa Mary ni Msimamizi wa Vipindi TBC Bibi Happinesi Ngasala.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Itilima Mkoa wa Simiyu. Mheshimiwa Njalu Silanga.leo Novemba 15/2017 katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma

Read More

WAZIRI MKUU AKUTANA AKUANA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI TANZANIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa China Nchini Tanzani Bibi Wang Ke nakufanya naye mazungumzo ya kikazi ofisini kwake Mjini Dodoma leo    Novemba 15/2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza jambo kutoka kwa Waziri wa Mambo Yandani (Mbunge) Mwigulu Nchemba wakati wa  kikao cha Tisa cha Bunge leo Novemba 15/2017 Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisikiliza jambo kutoka kwa Waziri wa Mambo Yandani (Mbunge) Mwigulu Nchemba wakati wa  kikao cha Tisa cha Bunge leo Novemba 15/2017 Mjini Dodoma.




Read More

Tuesday, November 14, 2017

SERIKALI YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MASUALA YA UKIMWI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa ufafanuzi wa masuala ya Ukimwi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI wakati wa warsha ya wajumbe wa kamati hiyo iliyofanyika Bungeni Dodoma Novemba 14, 2017.

Mkurugenzi wa Utafiti na Tathimini Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akiwasilisha mada ya hali ya UKIMWI nchini kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi wakati wa warsha kwa wajumbe wa kamati hiyo iliyofanyika tarehe 14 Novemba, 2017.
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Dr. Leonard Maboko akichangia hoja kuhusu masuala ya Ukimwi wakati wa Warsha ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI iliyofanyika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe. Daniel Mtuka akifafanua jambo wakati wa warsha kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu masuala ya Ukimwi nchini iliyofanyika Bungeni Dodoma Novemba 14, 2017.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe. Martha Mlata akichangia hoja wakati wa warsha iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi kuhusu masuala ya Ukimwi iliyofanyika Mjini Dodoma. 
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe.Zainab Bullu akifafanua jambo wakati wa warsha kwa wajumbe wa kamati hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe. Masoud Abdalla salim akichangia hoja wakati wa warsha ya Wajumbe wa kamati hiyo mjini Dodoma.

Read More

MAJALIWA AKUTANA NA WABUNGE WANAOTOKA MIKOA INAYOLIMA PAMBA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa kwenye ukumbi wa Msekwa, bungeni Mjini Dodoma kabla ya kikao kati ya Waziri Mkuu na Wabunge wanaotoka mikoa inayolima pamba Novemba  14, 2017.

Baadhi ya wabunge wanaotoka mikoa inayolima pamba wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Msekwa, bungeni mjini Dodoma Novemba 14, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 14, 2017. Kutoka kushoto ni John Heche wa Tarime Vijijini, Marwa Ryoba wa Serengeti na Esther Matiko wa Tarime Mjini.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokutana na wabunge wanaotoka  mikoa inayolima pamba kwenye ukumbi wa Msekwa, bungeni mjini Dodoma Novemba 14, 2017. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa.


Read More

Monday, November 13, 2017

WAZIRI MKUU BUNGENI LEO TAREHE 13 NOVEMBA,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungungumza na Mbunge wa Urambo Tabora, Magreth Sitta, nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Joseph Ngonyani(Maji Marefu) nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena, nje ya Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Meya wa Manispaa ya Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 13, 2017.


Read More

Sunday, November 12, 2017

IDARA YA MAAFA YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MAAFA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe. William Ngeleja akitoa maelezo ya awali kuhusu utendaji kazi wa kamati hiyo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 bungeni Mjini Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uratibu wa Maafa na namna Serikali inavyojenga uwezo wa Idara hiyo ili kuongeza tija wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa .

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu Maafa Novemba 12, 2017 bungeni Dodoma.

Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri  Mkuu  (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 Mjini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi Msuya akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Idara yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe hao iliyoandaliwa na Ofisi hiyo mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe.  Aida Kenani akichangia hoja wakati wa wakati  wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa bungeni mjini Dodoma.


Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa mhe. Abdallah Mtolea (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati na Watendaji wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi hiyo kwa lengo la kutoa uelewa wa masuala ya menejimenti ya maafa nchini.

Mmoja wa wawezeshaji kutoka Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ili kutoa uelewa wa masuala  ya Menejimenti ya maafa nchini Novemba 12, 2017.




Read More

IDARA YA MAAFA YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MAAFA

Ofisi ya Waziri Mkuu imeendesha warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Sheria Ndogo inayohusu Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Novemba 12, 2017 Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.William Ngeleja alieleza kuwa warsha hiyo itawajengea uwezo wajumbe wa Kamati hususani katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Warsha hii ni muhimu kwa wajumbe wa kamati kwani itaongeza uelewa kuhusu sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 pamoja na dhana nzima ya Menejimenti ya Maafa"

Akifanua mhe.Ngeleja amesema warsha hiyo itasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kamati hasa katika kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya maafa.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagamaaliwaeleza wajumbe kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini ili kujenga uwezo wa Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali pindi maafa yanapotokea hivyo warsha hii inatija kwa wajumbe wote.

"Warsha hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wajumbe kuhusu namna bora ya kupambana na majanga yanapoytokea nchini na madhara yake, vyanzo na sababu za kutokea, hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia, kupunguza  madhara, kujiandaaa , kukabili na kurejesha hali katika ubora zaidi" Alisisitiza Mhe. Mhagama.

Sambamba na hilo Mhe. Mhagama alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini kwa kuanzisha Idara ya uratibu wa maafa inayotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Pamoja na hatua hizo Serikali ina sera ya Taifa ya Usimamizi wa maafa ya mwaka 2004 ambayo inaeleza hatua na majukumu ya wadau mbalimbali katika shughuli za Manejimenti ya maafa na kutoa muongozo wa utekelezaji wake.

Aidha mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mhe.Elibariki Kingu alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendesha warsha hiyo na kushauri serikali kuwekeza zaidi katika kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza hapo nchini.

AWALI
Mada zilizowasilishwa katika warsha hiyo zilijikita katika Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa Maafa hapa nchini ikiwa ni moja ya jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuwajengea uwezo wadau na wananchi kwa ujumla ili kuweza kuyakabili maafa pindi yanapotokea. Warsha ilikuwa ya siku moja iliyojumuisha wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu masuala ya Menejimenti ya Maafa iliyofanyika Bungeni Dodoma.

Read More

Friday, November 10, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI MJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi wakati alipomtembelea Waziri mkuu ofisini kwake mjini Dodoma leo Novemba 10/2017 kwa mazungumzo ya kikazi.Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera Bunge,Kazi Ajira,Vijana na Walemavu Jenista Mhagama

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimfafanulia jambo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara Joyce Sokombi.(chadema) wakati wa Majadiliano ya Mapendekezo ya Mpango  wa Taifa wa Fedha kwa Mwaka 2018/2019 bungeni Dodoma leo Novemba 10/2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Martha Mlata (CCM) wakati wa Majadiliano ya Mapendekezo ya Mpango  wa Taifa wa Fedha kwa Mwaka 2018/2019 bungeni Dodoma leo Novemba 10/2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsalimia Mtoto Ivan (miezi7)akiwa katika Viwanja vya Bunge na Mama yake Mariam Zablon kutoka Bukombe mkoani Geita walipotembelea bungeni Dodoma leo Novemba 10/2017 kujionea shughuli za Bunge.

Read More

Thursday, November 9, 2017

HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesisitiza kwamba vyombo vya dola vya ndani ya nchi havijashindwa kuchunguza matukio ya kihalifu yaliyotokea nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na subira.

Amesema Serikali hairidhishwi na matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa, ambayo yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini na baadhi yake yamesababisha vifo na wengine kujeruhiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 9, 2017) wakati akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.

Bw. Mbowe alitaka apew kauli ya Serikali juu ya hatua zilizochukuliwa kuhusu tukio la kushambuliwa na mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu, ambapo alishauri uchunguzi huo ufanywe na vyombo vya kimataifa, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa na vyombo vya ndani vya dola.

“Vyombo vya ndani vya dola vina uwezo mkubwa wa kusimamia usalama wa nchi na vinaendelea na uchunguzi wa matukio hayo yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa letu. Nawaomba wananchi waendelee kuwa na imani na vyombo vyetu vya dola na mara uchunguzi utakapokamilika taarifa itatolewa.”

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi waendelee kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa mbalimbali juu ya vitendo vya kihalifu vinavyotokea kwenye maeneo yao kwa lengo la kudumisha amani na utulivu nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma imeanza kutekelezwa kwa kuwapandisha madaraja watumishi wanaostahili sambamba na kulipa malimbikizo yao mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema baada ya kumaliza ulipaji wa malimbikizo ndipo Serikali itaendelea na hatua ya uboreshaji wa mishahara kwa watumishi wote wa umma, hivyo amewaomba waendelee kuwa na subira na imani na Serikali. Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi, Bw. Omary Kigua aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itapandisha mishahara ya watumishi wa umma.

Pia Waziri Mkuu amezungumzia changamoto ya masoko kwa mazao ya mbaazi na tumbaku ambayo yanashughulikiwa na Serikali na tayari baadhi ya nchi zimeanza kuonyesha nia ya kununua mazao hayo, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na uvumilivu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Bibi Munde Tambwe aliyeiomba Serikali kumpatia ufafanuzi juu ya kukosekana kwa soko la tumbaku ambayo imelundikana katika maghala na Bibi Pauline Gekul Mbunge wa Babati aliyelalamikia kukosekana kwa soko la zao la mbaazi.

Akizungumzia kuhusu zao la tumbaku, Waziri Mkuu amesema changamoto hiyo imetokana na wakulima wa zao hilo kuongeza uzalishaji tofauti na makubaliano yaliyofikiwa awali na wanunuzi. “Nawaomba wakulima waendelee kuwa wavumilivu Serikali inafanya mazungumzo na nchi za lran, Korea Kusini, Misri na Indonesia ili waweze kununua tumbaku hiyo na kuwaondolea usumbufu wakulima.”

Read More