Wednesday, November 15, 2017

KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR YAVUTIWA NA URATIBU WA AFYA MOJA TANZANIA BARA

Kamisheni ya Kukabiliana na maafa Zanzibar imevutiwa na shughuli za kuratibu maafa nchini zinazofanywa na serikali ya awam ya Tano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Idara ya Kuratibu maafa ikiwa ni pamoja na kuratibu Afya moja ambapo katika Dhana ya Afya Moja, sekta ya   afya ya binadamu, wanyama (pori na wafugwao) na mazingira, zinakuwa na mawasiliano ya karibu kiutendaji na kupanga  mikakati ya pamoja katika kujiandaa na milipuko ya magonjwa na kukabiliana nayo endapo itatokea.

Akiongea wakati wa  ziara ya Kubadilishana Uzoefu na Idara ya Kuratibu Maafa na Ofisi ya Waziri Mkuu,jijini Dar es salaam leo tarehe 15 Novemba 2017, Mkurugenzi Mtendaji Kamishseni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Shaban Mohamedi amebainisha kuwa kamisheni yake imevutiwa na jinsi idara ya maafa inavyoweza  kuimarisha juhudi na ushirikiano wa sekta mbalimbali katika maandalizi ya kuzuia,kujiandaa na kukabili  magonjwa ambukizi kwa kujumuisha sekta zote muhimu.

“Tutaupitia mpango mkakati wa Afya moja  ili nasisi tuanze juhudi za kuratibu Afya moja  kwani  Kamisheni inajukumu lakukabiliana na Maafa hivyo tutachukua juhudi za kuhakikisha na sisi Zanzibar tunashirikiana na wadau husika ili tuweze kutumia rasilimali ndogotulizonazo kuweza kukabili  magonjwa yatokayo kwa  wanyama kwenda kwa binadamu yanayoiathiri jamii ya Zanzibar” alisisitiza Khatibu

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya , alifafanua kuwa suala la Afya moja linaratibiwa na ofisi yake kupitia Dawati maalum kutokana na kuwa magonjwa ya mlipuko ni masuala mtambuka na yanahitaji rasilimali watu na fedha nyingi hivyo kwa uratibu wa pamoja inasaidia kuhakikisha sekta zote zinashirikiana kukabiliana na athari za magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

“Umuhimu huu wa Afya moja unatokana na ukweli kwamba magonjwa na athari nyingine za binadamu kwa kiasi cha asilimia 60 hadi 80 huusisha wanyama. Kwa kufanya hivi ufanisi huongezeka kwani mchanganyiko wa Wataalamu, wakifanya kazi kwa pamoja na ushirikianao mkubwa, huchukua muda mfupi, na matumizi ya raslimali chache kwa pamoja huleta matokeo mazuri zaidi” Alisema Msuya.

Mwaka 2013, aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya awamu ya nne, ya Jamhuriya MuunganowaTanzania, Dk. Ghalib Bilal alizindua mtandao wa afya moja jijini Arusha. Kufuatia uzinduzi huo, mwaka 2015 wadau kutoka sekta mbalimbali walikaa na kutengeneza mpango mkakati wa afya wa miaka mitano (2015 – 2020). Mpango huo umeainisha masuala yahusuyo afya moja, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa utaratibu wa kuratibu shughuli zote za afya moja katika idara ya kuratibu maafa katika ofisi ya waziri mkuu.


EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.