Tuesday, April 11, 2017

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI MHAGAMA OFISI KWAKE BUNGENI DODOMA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke alipomtembelea waziri Ofisini kwake Bungeni Dodoma Aprili 11, 2017.

Na Mwandishi wetu:
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke amesema nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika kutoa mafunzo maalum ya Menejimenti ya Maafa kwa wataalamu wetu.

Ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ofisini kwake mjini Dodoma.

Akielezea lengo la ziara hiyo, Balozi Cooke alisema Serikali yake inataka kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inajipanga kukabili na kurejesha hali pindi  yanapotokea maafa.

 “Masuala ya maafa yapo nchi nyingi ikiwemo kwetu Uingereza ingawa mafuriko na ajali za moto zimekuwa zikiikumbaa nchi yetu mara kadhaa.”Alisema Balozi.

Aliongeza kuwa,  Serikali ya Uingereza  imevutiwa na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kukabili na kurejesha hali ikiwa pamoja na  kuwasaidia wananchi na mali zao pindi yanapotokea maafa.

Kwa upande wake, Waziri Mhagama alimpongeza Balozi huyo kuona umuhimu wa kuja Tanzania na kuonesha nia ya kuisaidia nchi kwa namna mbalimbali.

“Nishukuru kipekee kwa ujio wako na kuona umuhimu wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika maswala mazima ya maafa na kumhakikishia kuwa Tanzania ipo tayari na itajiandaa kuwaunga mkono kwa utayari wa kuisaidia nchi”Alisema waziri Mhagama
Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke akiongea jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke alimtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.




EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.