Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Novemba 28, 2017) amefungua kongamano la Kitaifa la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Juliasi Nyerere jijini Dar es Salaam.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawavumilia watu wote wanaotumia vibaya fedha za umma ambazo zinapaswa kuleta maendeleo kwa wananchi, zikiwemo na za Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.
Amesema mfuko huo unalenga kufanikisha ukusanyaji wa fedha za kutosha amabazo ni muhimu kwa Taifa wakati huu tunapoazimia kumaliza ukimwi ifikapo mwaka 2030..
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo leo (Jumanne, Novemba 28, 2017) wakati akifungua kongamano la Kitaifa la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lililofanyika jijini Dar es Salaam.
“Nitoe wito kwa Bodi ya Mfuko huu na watendaji wake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu fedha hizi ili ziweze kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko huu. “
Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kutenga fedha za mfuko huo na kuhamasisha wananchi, wadau na sekta binafsi kuchangia mfuko huo muhimu.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kujenga nchi ya viwanda ili waweze kufikia uchumi wa kati, jambo ambalo haliwezi kufikiwa iwapo wananchi wake watakuwa hawana afya bora.
“Hatutaweza kufikia malengo haya kama Taifa iwapo watu wetu hawatakuwa na afya bora kwani nguvu kazi kwa ajili ya Tanzania ya Viwanda itatokana na wananchi wenye nguvu na afya bora.”
“ Hivyo kama Serikali tutahakikisha tunaendelea kutoa huduma bora za afya ili wananchi wetu waweze kuwa na afya bora. Tutaendelea kuwakinga wananchi wetu hususan ni vijana ili Taifa letu liwe na nguvu kazi ya kutosha hasa wakati huu tunapoanza mageuzi makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.”
Pia Waziri Mkuu amesema kwamba kwa sasa Watanzania wengi wana uelewa mkubwa wa ukimwi lakini changamoto iliyopo ni kubadili tabia na kuachana na tabia hatarishi zinazosababisha kupata maambukizo mapya.
Amesema jambo hilo ni hatari kubwa kwa nchi yetu kwa sababu bado wananchi wengi wanaendekeza tabia ya kuwa na wapenzi wengi tena kwa wakati mmoja na hakuna uaminifu katika ndoa.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu “changia mfuko wa udhamini wa udhibiti ukimwi, okoa maisha”.
Kongamano hilo lilihudhuliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Walemavu Bibi Stella Ikupa Alex, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile, Makamishna wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS).
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt Leonard maboko, Mwenyekiti wa Baraza la Wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA), wawakilishi wa wadau wa maendeleo na wadau wa ukimwi nchini.
|
Tuesday, November 28, 2017
TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WANAOTUMIA VIBAYA FEDHA ZA UKIMWI-MAJALIWA
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
11/28/2017 11:14:00 AM
TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WANAOTUMIA VIBAYA FEDHA ZA UKIMWI-MAJALIWA
OFISI YA WAZIRI MKUU
5.0
stars based on
35
reviews
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Novemba 28, 2017) amefungua kongamano la Kitaifa la maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lili...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
Timeline
-
▼
2017
(470)
-
▼
November
(60)
- SERIKALI HAIJARUHUSU KOZI ZA FOUNDATION CHUO KIKUU...
- WAZIRI MKUU ATAKA UDAHILI ELIMU YA JUU UONGEZWE
- MAJALIWA MGENI RASMI MAHAFALI YA 33 YA CHUO KIKUU ...
- WAZIRI MKUU AMKABIDHI IGP WALIOTAKA KUTOA SEMI TEL...
- WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA...
- MAJALIWA AWASILI SINGIDA
- TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WANAOTUMIA VIBAYA FEDHA ZA ...
- WAZIRI MKUU AKABIDHI KOMBE LA UBINGWA KWA TIMU YA ...
- MAKATIBU WAKUU OFISI YA WAZIRI MKUU WAKUTANA NA ME...
- TUTAMALIZA KERO YA MAJI TUNDURU-MAJALIWA
- WAZIRI MKUU AUNGANA NA WANASONGEA KUOMBOLEZA KIFO ...
- MAJALIWA: TANESCO KAWAHUDUMIENI WANANCHI VIJIJINI
- WAZIRI MKUU AKIWA KATIKA ZIARA YA KIKAZI NAMTUMBO,...
- CHUO KIKUU ARDHI MARUFUKU KUKODI MAKAMPUNI-MAJALIWA
- CHUO KIKUU ARDHI MARUFUKU KUKODI MAKAMPUNI-MAJALIWA
- WAZIRI MKUU AMPA OFISA ARDHI MWEZI MMOJA KUFIDIA W...
- WAZIRI MKUU AKABIDHI CARRY KWA TIMU YA AFISI KUU Z...
- WAZIRI JENISTA ATEMBELEA VITUO VYA HALI YA HEWA AR...
- WAZIRI MHAGAMA AITAKA HALMASHAURI YA BAHI KUKAMILI...
- WAZIRI MHAGAMA AITAKA HALMASHAURI YA BAHI KUKAMILI...
- WAZIRI MHAGAMA : UHABA WA SUKARI NCHINI WAPATA MWA...
- MAVUNDE: WATU WAKIKOSA MAADILI TAIFA LINAKUFA
- KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATE...
- WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA KATIBU ...
- WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA KATIBU ...
- SERIKALI YAKARABATI VYUO 10 KWA SH. BILIONI 12
- SERIKALI YATOA MAFUNZO KWA VIJANA ZAIDI YA 11,000
- MAJALIWA:MWENENDO WA UKUAJI UCHUMI WA TAIFA UNARID...
- MAJALIWA AAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE
- WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA KATIKA...
- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIJIBU MASWALI BUNGENI
- MALIASILI KAMILISHENI ZOEZI LA UWEKEJI ALAMA MAENE...
- MAJALIWA AKISALIMIAN NA WAGENI MBALIMBALI WALIOTEM...
- KILIMO WATAKIWA KUTAFITI MBEGU BORA ZA PAMBA-MAJALIWA
- KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR YAVUTIW...
- KAMISHENI YA KUKABILIANA NA MAAFA ZANZIBAR YAVUTIW...
- SERIKALI KUZINDUA RIPOTI YA UTAFITI WA KITAIFA WA ...
- SERIKALI KUZINDUA RIPOTI YA UTAFITI WA KITAIFA WA ...
- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKISALIMIANA NA WATU M...
- WAZIRI MKUU AKUTANA AKUANA NA BALOZI WA CHINA HAPA...
- SERIKALI YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA KUD...
- MAJALIWA AKUTANA NA WABUNGE WANAOTOKA MIKOA INAYOL...
- WAZIRI MKUU BUNGENI LEO TAREHE 13 NOVEMBA,2017
- IDARA YA MAAFA YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI ...
- IDARA YA MAAFA YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI ...
- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA KATIBU MKUU...
- HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA
- WAZIRI MKUU BUNGENI LEO TAREHE 09 NOVEMBA,2017
- KATIBU MKUU MPYA APOKELEWA KWA SHANGWE DODOMA
- BUNGENI LEO TAREHE 08 NOVEMBA,2017
- MAWAZIRI MSITOE MATAMKO YASIYOTEKELEZEKA-MAJALIWA
- WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA WADAU WA MASUALA YA AJIR...
- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIWASIKILIZA MAWAZIRI
- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA MAAD...
- WAZIRI MKUU AKIWA MKOANI LINDI KWA ZIARA
- ‘RUANGWA INAHITAJI SEKONDARI YA WASICHANA’
- WATAKAOKWAMISHA MALIPO YA KOROSHO KUKIONA-MAJALIWA
- WAZIRI MKUU AHIMIZA LINDI WAJIPANGE MAANDALIZI YA ...
- WAZIRI MKUU AWASILI TOKEA NCHINI CANADA
- HABARI PICHA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO W...
-
▼
November
(60)
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.