*Ataka
viongozi wote wasimamie kilimo hicho
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Bodi ya Pamba ifanye kazi kwa karibu na Wakuu wa Mikoa
ili kuhakikisha msimu huu zao hilo linafikia malengo ya uzalishaji.
Ametoa
agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Januari 18, 2019) wakati akizungumza na Wakuu wa
mikoa nane ya Mara, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga,
Singida na Tabora inayolima pamba pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga.
Waziri Mkuu ameendesha kikao hicho kwa njia ya video (video conference) kutokea
ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ili aweze kupata picha halisi ya kilimo cha
pamba na hatua zilizofikiwa hadi sasa katika msimu huu wa kilimo.
“Lego letu mwaka huu 2019 ni kuzalisha tani zisizopungua 600,000. Wote
mmeeleza kuwa wakulima wako kazini, pamba inalimwa, mnachosubiria ni dawa za
kuuza wadudu waharibifu, na Bodi imeeleza kuhusu upatikanaji wa dawa hizo.”
Waziri
Mkuu pia amesema viongozi wote wanapaswa kuwa karibu na wakulima ili waweze
kubaini shida zao na kuzitatua kwa haraka. “Viongozi wote huko tuliko, zaidi ya
asilimia 75 ya wa wananchi wetu ni wakulima. Kwa hiyo basi, tunapaswa tutenge
asilimia zaidi ya 50 ya muda wa wetu kwenye mpango kazi ili tuweze kusimamia
kilimo,” amesema.
“Wakuu
wa mikoa peke yenu hamuwezi kufika kila mahali. Ni lazima maafisa ugani, maafisa
kilimo na maafisa ushirika kwenye Halmashauri zetu waende kwa wakulima. Nikisema
viongozi siyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya peke yao, Wizara nayo ina jukumu la kusimamia,
viongozi wa AMCOS, vyama vikuu vya ushirika wote wawajibike kushirikiana na Serikali,
waangilie ni nini tufanye ili kumkomboa mkulima.”
“Warajis wasaidizi, Ma-Ras wasaidizi wanaohusika na kilimo ni lazima washirikane kuhakikisha wakulima wetu wanajikwamua kutoka hapo walipo,” amesisitiza.
Mapema, akitoa taarifa ya maandilizi ya kilimo cha pamba kwa
msimu huu, Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba alisema hadi sasa wamekwishasambaza tani
27,000 za mbegu ambao ni zaidi ya asilimia 37 ikilinganishwa na usambazaji wa
mbegu wa msimu uliopita.
“Hadi
sasa mikoa yote imepata mbegu na zimeshapandwa na hali ya uotaji ni asilimia
100 kwani hatujapata malalamiko yoyote,” alisema.
Kuhusu
dawa za viuadudu, Mkurugenzi huyo alisema wameshanunua chupa milioni sasa na
vinyunyizi 23,000.
Wakichangia
mjadala kwenye kikao hicho, kwa nyakati tofauti, Wakuu hao wa mikoa waliunga mkono
dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kufufua ushirika kama njia pekee ya
kumkomboa mkulima.
Walisema
kuna haja ya kutafuta njia mbadala ya kuwatoa wakulima wa pamba kwenye
utegemezi wa mikopo ili waweze kupata mbegu na pembejeo na badala yake wapewe
elimu ya kujiwekea akiba tangu wanapovuna na lkuuza mazao yao.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.