Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, amekagua hatua ya ujenzi wa
jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo eneo la Njedengwa
Jijini Dodoma na kusema kuwa serikali imedhamiria shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka
huu kufanyika kwenye jengo hilo jipya la Tume hiyo.
Amebainisha hayo wakati alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya Ujenzi wa
majengo ya Tume hiyo, leo tarehe 10 Machi, 2020, ambapo amekagua hatua za ujenzi wa ofisi za Tume hiyo kwa
kukagua Jengo Kuu la Ofisi, Jengo la
kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa.
Kukamilika kwa majengo hayo itakuwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwezi Novemba
mwaka jana, ambaye aliitaka tume hiyo kuhakikisha ujenzi wa Ofisi za Tume hizo unakamilika
kwa wakati, ili shughuli za uchaguzi Mkuu wa mwaka huu zifanyike kwenye majengo hayo.
Chuo kikuu- Ardhi na Kampuni ya Ujenzi ya Jeshi la Kujenga
Taifa- SUMA JKT CCL ndio wanaohusika na shughuli za ukandarasi wa majengo hayo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni idara huru iliyoanzishwa mwaka
1993 kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1997, ambapo kwa kipindi chote hicho tangu kuanzishwa kwake Tume hiyo
haijawahi kumiliki Jengo lake lenyewe, hivyo mnano mwaka 2016, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikubali ombi la Tume hiyokujenga
jingo lake.
MWISHO.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.