Makamu wa Pili wa Rais,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah ameeleza kuwa Nchi
ya Tanzania imejipanga kufanya ya sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa
njia ya kidijitali ambapo itarahisisha ukusanyaji wa taarifa wakati wa zoezi
hilo.
Ametoa kauli hii wakati akifunga
mafunzo ya Wakufunzi wa sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ngazi ya Taifa
uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani
Iringa tarehe 01 Julai, 2022.
Makamu wa Pili wa Rais alisema
kuwa, sensa ya mwaka huu itaendeshwa kwa mifumo ya kitehama ambapo itakuwa ni
mara ya kwanza kwa nchi kuwa na mfumo mpya utakaongeza ufanisi.
“Sensa ya mwaka huu ni ya sita
itakayobebwa na upekee wa aina yake kwani inaunganisha matukio mawili makubwa
ya kitaifa ikiwemo la ukusanyaji wa taarifa za majengo yote nchini pamoja na
taarifa za idadi ya watu,” alieleza.
Aidha alisema hadi sasa
maandalizi yake yamefiki asilimia 87 na hii inaonesha ni hatua nzuri kwa taifa
hivyo watu waendelee kupewa elimu kwa wingi.
“Kuhesabu watu kitaalam
itasaidia kupata taarifa kwa urahisi, na kazi hii itafanyika kwa umakini mkubwa
hivyo tuifanye kwa weledi na viwango vinavyotakiwa,”aliongezea Mhe. Abdallah
Sambamba na hilo alitoa rai
kwa wakufunzi hao kuendelea kuzingatia uzalendo katika utekelezaji wa majukumu
yao.
“Wahitimu wetu wote zingatieni
uzalendo na muwe vielelezo vizuri kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha
wananchi kujitokeza katika zoezi hili la sensa ili kuleta matokeo makubwa,”alisisitiza.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe.
George Simbachawene alieleza kuhusu utekelezaji wa zoezi la Operesheni Anwani
za Makazi kuwa umefikia asilimia 95, hii
ikiwa ni muunganiko wa utekelezaji wa shughuli zote zilizopangwa.
Aidha alisema kuwa, Kazi
zinazoendelea kufanyika kwa sasa ni kuhakiki na kusafisha taarifa za anwani
pamoja na kuweka miundombinu ya anwani za makazi inayojumuisha nguzo za majina
ya barabara na kubandika vibao vya namba za nyumba/anwani kwenye majengo.
“ Licha ya kuwa hatua iliyofikiwa
katika utekelezaji wa Operesheni hii kuwezesha zoezi la Sensa kufanyika kwa
tija, Operesheni hii imeacha alama katika kuimarisha ustawi wa jamii, Vijiji na
Miji, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mikoa na Taifa katika nyanja mbalimbali
ikiwemo Uchumi wa Kidijitali,”alisema Mhe. Simbachawene
Kwa upande wake Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande alisema kuwa, zoezi la sensa ya
watu na makazi ni nyenzo muhimuu kwa kuzingati tija iliyopo hususan katika masuala
ya mipango ya maendeleo ya nchi yetu kwa kuzingatia uwepo wa bajeti yenye
kukidhi mahitaji yaliyopo.
“Matokeo ya sensa ya mwaka
2022 yatatoa mwelekeo mzima wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Samia
Suluhu Hassan kuhusu utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwa wananchi wetu
kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, na matokeo haya ni
nyenzo muhimu kwa wizara yangu kwani yatasaidia kufuatilia utekelezeaji wa
bajeti katika sekta zote,”alisisitiza.
AWALI
Wakufunzi zaidi ya 500
wamehitimu mafunzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa ngazi ya Taifa yaliyofanyika
katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa tarehe 01 Julai,
2022 ambapo wakufunzi hao walitumia jumla ya siku 21 kupatiwa ujuzi huo.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.