Serikali yahimiza jamii kuanzia ngazi ya familia kuimarisha mfumo wa
ushughulikiaji wa matukio ya ukatili dhidi ya watoto ndani na nje ya shule
unaowajumuisha wasimamizi wa shule, wazazi, walezi na jamii kwa lengo kuendelea
kutokomeza matukio ya ukatili nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe.
George Simbachawene katika Mkutano wa Kitaifa wa tafakuri ya Utekelezaji wa
Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto
(MTAKUWWA) uliofanyika katika Ukumbi wa Saint Gaspar Jijini Dodoma.
Waziri ameeleza kwamba Mfumo
wa Ushughulikiwaji wa matukio ya ukatili utasaidia Taifa kupunguza kwa kiasi
kubwa changamoto iliyopo katika jamii ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa
Watoto.
“tuendelee kuunga mkono juhudi
za Serikali kwa hali na mali ili kuhakikisha makundi yote ndani ya jamii
yanalindwa dhidi ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto alisema,”
alisema Waziri Simbachawene.
Akieleza kuhusu Mkataba wa
Kimataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1989, wa Sera ya Maendeleo ya Mtoto 2008 na
Sheria ya Mtoto Na. 21, 2009, ambao unaoelezea masuala ya ukatili kwa watoto ni
kinyume cha haki zao za msingi za kuishi, kuendelezwa, kulindwa na
kutokubaguliwa.
Aidha umeeleza kuwa,vitendo
vya ukatili vinarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kufikia Malengo ya
Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto wa
mwaka 1989 ambayo nchi imeridhia kutekeleza.
Waziri amehimiza kuendeleza juhudi
za kukabiliana na ukatili huo katika zama za utandawazi kuwa na msukumo mpya na
wa pamoja ili kuwalinda watoto dhidi ya ukatili.
Amesema kuwa, athari za
utandawazi zimedhoofisha mifumo ya ulinzi na usalama wa watoto hivyo kufanya
kundi hilo kutokuwa salama kwani tatizo la ukatili bado ni changamoto katika
ngazi zote.
Kwa upande wake, Waziri wa
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na
Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima
amesema wizara ya Maendeleo ya jamii imekuwa ikiratibu utekelezaji wa MTAKUWWA
toka kuzinduliwa kwake mwaka 2016, na baada ya kukamilika kwake Wizara pamoja
na Wadau wa maendeleo walifanya tathimini ya utekelezaji wake kuanzia 2017/2018
hadi 2021/2022 kupitia Mtaalam mwelekezi Chuo Kikuu cha Dodoma.
Waziri amesema taarifa ya
tathimini imekamilika na imebainisha utekelezaji wa MTAKUWWA kwenye maeneo yote
nane yalliyopo kwenye mpango huu, na imebainishwa maeneo muhimu yatakayoenda
kutekelezwa kwenye mpango kazi ujao.
“Niwaombea wadau tuwe na
subira tukiwa tunaendelea mapitio ya pamoja mpaka itakapotangazwa kwamba
serikali pamoja na wadau,”aliomba Waziri Gwajima
Naye Mkurugenzi wa Shirika la
ICS Tanzania Bwn. Kudely Sokoine Joram amesema wataendelea kuunga mkono
jitihada za Serikali katika kuhakikisha mapambano haya yanatokomezwa huku akiipongeza
Serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na changamoto ya ukatili wa
makundi haya muhimu huku akitaja maeneo muhimu ikiwemo la kuimarisha mifumo ya
ulinzi wa Wanawake na Watoto, kujenga uwezo wa Kamati za ulinzi wa Wanawake na
watoto pamoja na kusaidia uratibu wa Masuala yote.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.