Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera
Bunge na Uratibu wametakiwa kutumia sheria, kanuni na miongozo ya Serikali
pamoja na Busara katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Hayo yamesema na aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi Bw. Kaspar Mmuya.
Bw. Mmuya alisema ameitumikia Ofisi hiyo
na kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja kwa lengo la kuleta matokeo chanya.
“Kwa majukumu ya Ofisi hii jinsi yalivyo
yalitupa nafasi sisi wengine ya kujua wizara nyingine zinafanya nini katika
kutekeleza majukumu ya Serikali kwa ujumla,”alisema Katibu Mkuu huyo.
Pia amewahimiza watumishi wa Ofisi
hiyo kuishi kwa upendo na kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu hatua
itakayochochea maendeleo ya Taifa na shughuli za Serikali kufanyika katika hali
ya ubora na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Sambamba na hilo, Bw. Mmuya alimshukuru
Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu kwa
kumfundisha, kumuongoza na kumpa ushirikiano wakati wote alipokuwa akitumikia
nafasi ya Naibu Katibu Mkuu katika ofisi hiyo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu alisema kuwa Katibu
Mkuu Mmuya alikuwa akitekeleza majukumu yake kwa matokeo hivyo watumishi
kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kufanya kazi kama timu katika
kuitumikia Nchi, kuishi na watu vizuri.
“Tujitahidi kila wakati kufanya
kazi kwa matokeo, uliyaishi matokeo na unaendelea kutukumbusha tuyaishi hayo,
kila mtu ana nafasi yake lakini lazima kuheshimiana na kujua umuhimu wa
kuwajibika, tuendelee kufanya kazi kwa matokeo weledi ushirikino na nidhamu
sisi ni timu moja tushirikiane.” Alisisitiza Dkt. Jingu.
Akiongea kwa niaba ya watumishi wa Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Katibu wa TUGHE tawi la Ofisi
hiyo Bw. Dotto Kyaolang amemshukuru Katibu Mkuu Mmuya kwa kutoa dira ya
utendaji kazi na kumtakia afya njema na utendaji mwema katika kituo chake kipya
cha kazi.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.