Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amewataka wananchi kuondoka katika maeneo hatarishi ili kujikinga na mafurikio ya mvua za vuli
zinazoendelea kunyesha.
Kauli hiyo ameitoa wakati
alipotembelea na kujionea maeneo yaliyokubwa na mafuriko ya mvua katika
Halmashauri ya Mlimba Mkoani Morogoro ambapo amewaomba wananchi kuendelea
kufuatilia na kusikiliza ushauri wa serikali.
Niwaombe wananchi tuendelee
kushikamana ili kupambana na majanga ya Mvua na Mafuriko, ambayo yameleta
kadhia kubwa sana kwa wananchi.
“Serikali imetengeneza Mpango
wa Dharura wa kukabiliana na mvua za El Nino na mvua za Masika, ambapo serikali
itafanya kila linalowezekana kuzuia madhara yasitokee na hasa maisha ya
watanzania,” alisema Waziri Mhagama
Ameongeza kusema mafuriko ya
maji yamesababisha udongo kumomonyoka na kuharibu miundo mbinu ya reli na
kuleta madhara mengine mengi niwaombe wanamlimba tuendelee kuangalia na
kusikiliza ushauri wa serikali.
“Serikali itaendelea kuhakikisha
inapambana dhidi ya magonjwa ya Mlipuko na uhaba wa chakula na madhara mengine ambayo yameathiri
wananchi, serikali itakuwa pamoja na nyinyi katika kutatua kadhia hizo alibainisha,”
Waziri Mhagama
Niwaombe wananchi tuendelee
kumuomba mwenyezi Mungu hali iliyopo mbele yetu iweze kupita kwa haraka na ipite
kwa usalama mkubwa.
Ameeleza kwamba katika utabiri wa hali ya hewa
unaoendelea kutolewa unaonesha mvua hizi zinaendelea kunyesha hivyo ni vyema
tukaendelea kujichukulia tahadhari sisi wenyewe.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya
ya Kilombero Mhe. Dustan Kyobya amesema changamaoto ya Mawasiliano ya barabara
kwa watu wa Masagati na Utengule kwao wamekuwa kisiwa kutokana na miundo mbinu
ya barabara kutopitika, lakini pia Mawasiliano kati ya Jimbo la Ifakara na Mlimba
ambazo zinatengeneza wilaya ya kilombero nayo ni magumu.
Aidha Miundo mbinu ya reli ilidondokewa
na udongo na kusababisha kukatika kwa makalvati ya reli hivyo kusababisha
usafiri wa kutoka Mlimba kuelekea makambako kutokuwepo.
“Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuma ndege kwa ajili
ya kuokoa watu waliokwama na kuruhusu treni ya Mwakyembe kuanza kubeba abiria ili kurahisisha
mawasiliano,” alisema Mkuu wa wilaya
Awali Bi, Zainabu Makenjula Mkazi
wa Mlimba ameomba serikali kushughulikia swala la barabara kwa wakati ili
kurahisisha mawasiliano na kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli za
uzalishaji kwa sababu kuna maeneo magari wala pikipiki haviwezi kupita.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.