Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Williamu Lukuvi amesema ujenzi na uimarishaji wa wa miundo mbinu ya Maji Kata ya Mbezi ni kielelezo tosha kinachoonesha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo.
Waziri ametoa kauli hiyo
wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ambapo
ametembelea na kujionea Mradi wa Maji Mshikamano ulipo Kata ya Mbezi Katika
Wilaya ya Ubungo Jijini Dar e salaam na baadae kufanya Mkutano wa hadhara
Mburahati.
Shida ya maji Kata ya Mbezi
ilikuwa tatizo kubwa hivyo kukamilika kwa Mradi wa Maji niliotembelea kwa
100% utahudumia watu zaidi ya laki mbili.
“Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu
Hassan ametegua kitendawili hicho kwa Wananchi wa Ubungo kupata Maji safi na salama
ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake hivyo niwape shime Wananchi
muendelee kutangaza kazi njema zinazofanywa na Serikali,” alisema Waziri Lukuvi.
Kazi hizi zinazofanywa na Serikali
zinapaswa kuonekana na kutangazwa ili Watanzania wengine waone kazi mbalimbali
kwa mifano na Falsafa ya Mhe. Rais ya Kazi iendelee inaendelea kutekelezwa kwenye miradi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) Ubungo amesema
kupitia mradi wa Metroplitan Development Project (DMDP) Awamu ya Pili utajenga
kingo za Mto Gide na Mto China huko Makurumula,
Aidha kwa kupitia Mradi wa (DMDP)
kwa upande wa Ubungo kuna barabara 21 zitakazojengwa ikiwemo barabara nne kubwa
katika Kata ya Kimara ambazo ni barabara ya lami Suka, Barabara ya Mlingo,
barabara ya Milenia ya tatu, alisema Waziri Kitila.
Naye Mhe. Issa Mtemvu (Mb) Kibamba
amesema Wilaya ya Ubungo ilikuwa na wastani mdogo wa upatikanaji wa maji,
lakini Mhe. Rais amechukua kilio cha wakazi wa Ubungo na leo miradi
imekamilika.
“Serikali haikuwaacha Wananchi
wa Goba na viunga vya Salasala katika ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo
wa lita zaidi ya milllioni sita eneoTegeta A hivyo tunamshukuru sana Mhe. Rais,
Dkt Samia,” alisema Mhe Mtemvu
Wabunge tumepata bahati
tunaomba fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo Serikalini na tunazipata,
ahadi yetu ni kuendelea kumunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani.
Awali Mkuu wa wilaya ya Ubungo
Mhe Hassan Bomboko amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Mhe. Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa na zuri kwa kuleta miradi ya maendeleo ambayo
imechagiza mabadiliko makubwa kwa sekta mbalimbali.
Wananchi wa wilaya ya Ubungo
wana deni kwa Mhe, Rais kutokana na kazi kubwa ya utekelezaji wa Miradi ya
Maendeleo iliyofanya na Serikali ya Awamu ya Sita, kwa dhamira ya kweli na ya
dhati.
“Hakuna Kata ambayo haijaguswa
kabisa kwa upande wa mradi iwe ni upande wa Elimu, Maji, Barabara Afya au Miradi
mengine ya Maendeleo” alisema, Mkuu wa wilaya Bomboko.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.