Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu imezindua mradi wezeshi wa “Ramani Zetu, Sauti Zetu”, unaolenga kuwajengea uwezo Wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani katika kukabiliana na Majanga.
Akizungumza
katika Uzinduzi huo uliofanyika leo Jijini Morogoro Mkurugenzi Msaidizi wa
Operesheni na Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge Uratibu na
Wenye Ulemavu) Kanali Selestine Masalamado amesema, mradi huo umekuja wakati
mufaka ambao jitihada kubwa zikiwa zinaendelea za kuzuia majanga ya asili
maeneo mbalimbali ya nchi.
Aidha,
ameeleza kuwa “tunahitaji uwepo wa data sahihi za wakati bila kusahau
ushirikishwaji wa moja kwa moja wa jamii katika kuendelea kukabiliana na
majanga ya asili na athari zake”
“Mpango
huu unaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 inayolenga kujenga taifa
lenye jamii imara yenye uwezo wa kutumia maarifa ya teknolojia katika kufanya
maamuzi ya maendeleo” aliongeza Kanali Masalamado.
Naye,
Mkurugenzi wa Taasisi ya OpenMap Development Tanzania (OMDTZ) Bw. Innocent
Maholi, amesema Mradi huo unalenga kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema,
ikiwa ni pamoja maandalizi na usimamizi wa maafa kwa kutumia teknolojia na
ushiriki wa wananchi katika ukusanyaji wa taarifa muhimu za maeneo yao.
“serikali
itaendelea kuuunga mkono juhudi hatua za usimamizi madhubuti wa maafa ambazo
sehemu muhimu ya safari ya kuelekea maendeleo endelevu na uchumi imara wa
wananchi,” alibainisha

EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.