Idara
ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye
Ulemavu imewajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Wataalamu ya Usimamizi wa Maafa
ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa ili kuhakikisha jamii inakuwa stahimilivu
wakati wa majanga.
Elimu
hiyo imetolewa na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa kikao
cha kupitia Rasimu za Nyaraka za Usimamizi wa Maafa za Halmashauri ya Wilaya ya
Nkasi kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa wilayani humu ikiongozwa na na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Kikao
hicho kimeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye
Ulemavu kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Halmashauri ya
Wilaya ya Nkasi kikilenga kuwapitisha katika nyaraka zilizoandaliwa kwa ajili
ya matumizi ya Halmashauri ambazo ni Tathmini ya Vihatarishi vya Majanga,
Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Majanga, Mpango wa Kujiandaa
na Kukabiliana na Maafa pamoja na Mkakati wa kupunguza vihatarishi vya maafa.
Akitoa
neno la shukran mara baada ya kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Bw. Eliud Njogellah amepongeza kazi iliyofanyika
na timu ya kuandaa nyaraka hizo huku akieleza kuwa zimekuja kwa wakati sahihi
ambapo Halmashauri imekuwa ikikumbwa na majanga na maafa mbalimbali hivyo
zitatumika kwa uzito wake na tija iliyokusudiwa.
.jpg)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.