WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wakazi wa mji wa Songea na kata ya Matogoro
kuuaga mwili wa aliyekuwa Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki katika ibada iliyofanyika kwenye parokia ya Mt. Teresia wa Mtoto
Yesu iliyoko Matogoro, mjini Songea.
Waziri Mkuu
ambaye ameshiriki msiba huo kwa niaba ya Serikali, pia alishiriki mazishi ya Kapteni Mhaiki ambaye
pia alikuwa rubani wa ndege za Serikali yaliyofanyika kwenye makaburi ya
parokia ya Matogoro.
Akizungumza
kwenye ibada ya mazishi mara baada ya kutoa heshima za mwisho, leo jioni (Jumatano,
Januari 4, 2017), Waziri Mkuu aliwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais,
Mama Samia Suluhu Hassan.
“Msiba huu ni
wetu sote na umetugusa wote. Ni
msiba mzito kwa wanafamilia na kwa Serikali pia. Kapteni Mhaiki amekuwa rubani
wa ndege za Serikali kwa muda mrefu na amewaendesha viongozi wa kitaifa kuanzia
awamu ya kwanza hadi awamu ya tano. Kwa niaba ya Serikali tunawapa pole sana,”
amesema.
“Ninawaomba
wafiwa wote hasa mke wa marehemu na watoto tushikamane katika kipindi hiki na
tuendelee kuwa wavumilivu huku tukimuombea Baba yetu apate pumziko la milele,”
amesema.
Kapteni
Mhaiki alifariki dunia Desemba 31, 2016 katika hospitali ya Agha Khan jijini
Dar es Salaam. Alilazwa katika hospitali hiyo, kabla ya sikukuu ya Krismasi,
kwa ugonjwa wa saratani ya ini.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.