WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali chini ya Mheshimiwa Rais
Dkt. John Magufuli inautashi wa dhati wa kuboresha mazingira ya uwekezani na
biashara nchini kwa kuondoa rushwa na urasimu katika sekta ya umma, hivyo
amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Mauritius kuja nchini.
Amesema
Tanzania imefanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa kubadili mifumo yake ya
kisheria, kitaasisi na kifedha ili kuhakikisha wawekezaji wanahudumiwa ipasavyo
na kupewa umuhimu wanaostahili kwani ni wadau muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Waziri
Mkuu amesema hayo jana (Alhamisi, Machi 23,2017) wakati akifungua kongamano la Biashara na
Uwekezaji kati ya Tanzania na Mauritius lilifanyika katika Hotel ya Labourdonnaise mjini Port
Louis nchini Mauritius.
Kongamano hilo liliandaliwa na Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC).
Alisema
Tanzania ina uchumi imara unaofuata misingi ya soko huria, ambapo mwekezaji ana
uhuru wa kufanya biashara bila ya kuingiliwa na Serikali, hivyo sekta binafsi imepewa
kipaumbele katika shughuli za kiuchumi na kibiashara nchini.
“Kwa niaba
ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli nawakaribisha
kwa mikono miwili kuja na kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali
zikiwemo za viwanda na utalii na kutembelea vivutio vya utalii na kupata burudani
ya aina yake na kwa wafanyabiashara Tanzania ni mahali pazuri kwa kuwekeza,”
alisema.
Alisema TIC
na Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar kwa pamoja vimeweka taratibu ambazo
zinamwezesha mwekezaji kupata mahitaji yake muhimu ya kuwekeza katika kituo
kimoja (One stop Centre).
Alibainisha
baadhi ya mahitaji hayo kuwa ni huduma za kusajili kampuni, kodi, uhamiaji,
leseni za biashara, ardhi pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu uwekezaji.
Hali ambayo inachangia Tanzania kupata wawekezaji wengi kutoka ndani na nje.
Waziri Mkuu
alisema wawekezaji wanaokuja kuwekeza Tanzania wanatoka katika mataifa
mbalimbali kama Marekani, Canada, Afrika Kusini, Kenya, Autsralia, Umoja wa
Falme za Kiarabu (UAE) na hivi karibuni wanatarajia wawekezaji kutoka nchini
Mauritius.
“Ujio wa
wawekezaji hawa haukuwa wa bahati bali ni kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa
na Serikali pamoja na suala zima la soko
kubwa la bidhaa zao na huduma. Soko hili linalozidi watu milioni 300 katika
nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika linatoa uhakika wa soko kubwa kwa
mwekezaji yeyote anayekuja Tanzania kuwekeza,”.
“Kuwekeza
nchini Tanzania kunampa fursa mwekezaji kupata fursa maalumu kupitia Jumuia ya
Afrika Mashariki (EAC) na ile ya Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na soko la
nchi ambazo hazipakani na bahari. Nchi ambazo Tanzania ina mahusiano nazo
mazuri ya kibiashara ni Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na Zambia.
Waziri Mkuu
aliongeza kuwa katika kuheshimu wawekezaji Tanzania imesaini mikataba mbalimbali inayolenga
kuwalinda popote walipo kama Multilateral
Investment Guarantee Agency (MIGA) na Africa
Trade Insurance Agency.
Alisema
Tanzania mbali ya hali ya amani na utulivu wa kisiasa, pia imebarikiwa kuwa na
utajiri mkubwa wa rasilimali asilia ambazo zinatoa fursa nzuri kwa mwekezaji.
“Hii ni pamoja na ardhi yenye rutuba nzuri kwa kilimo, madini ya kila aina
kuanzia dhahabu, almasi, makaa ya mawe, tanzanites, chuma na gesi asilia,”.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Mauritius
Mheshimiwa Pravind Kumar Jugnauth, Prime Minister of the Republic of
Mauritius; Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius Bw. Seetanah
Lutchmeenaaraidoo, Waziri wa Fedha na
Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed,
Balozi wa Heshma wa Tanzania nchini Mauriutius Bw. Cliford Tandali.
Wengine ni
Mwenyekiti wa Taasisi
ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye,, Executive
Director of Tanzania Investiment Centre; Mkurugenzi
Mtendaji wa
TIC Bw. Clifford Tandar pamoja na Maofisa wa Serikali ya Tanzania na Mauritus
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.