§ Awataka waje kujenga viwanda vya sukari, nguo na samaki
SERIKALI imepanga kuondoka katika uchumi wa chini na
kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025
ambapo katika kufikia azma hiyo imeweka juhudi kwenye uanzishwaji wa viwanda
mbalimbali kuanzia vidogo hadi vikubwa.
Mpango wa kufikia uchumi wa kati unalenga kuiwezesha
serikali kujitegemea na tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuweza kufikia
azma hiyo.
Dira ya Taifa ya Maendeleo, imeainisha malengo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenge uchumi imara wenye uwezo wa kukabiliana
na ushindani.
Katika kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa Serikali imeweka sera na mazingira mazuri kwa
ajili ya kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye viwanda.
Hivi karibuni
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikwenda nchini Mauritius kumwakilisha Rais Dk.
John Magufuli kwenye uzinduzi wa Jukwaa
la Uchumi Barani Afrika (AEP).
Baada ya kumaliza uzinduzi huo Waziri Mkuu alipata
fursa ya kutembelea viwanda mbalimbali nchini Mauritius na kuhamasisha
wawekezaji waje nchini ili kuongeza uzalishaji utakaokuza uchumi na kuongeza
pato la taifa.
KIWANDA CHA
SUKARI CHA ALTEO
Akiwa kiwandani hapo Waziri Mkuu alipata maelezo ya
uendeshaji wake kuanzia hatua ya utayarishaji wa mashamba ya miwa hadi
uzalishaji wa sukari.
Waziri Mkuu alifurahishwa na teknolojia ya kisasa
inayotumika kiwandani hapo hali iliyomfanya ashawishike kuwashawishi wawekezaji
hao kuja nchini kupanua uwekezaji kwa kuongeza mashamba ya miwa na uzalishaji
wa sukari.
Kiwanda cha sukari kinachomilikiwa na kampuni ya
Alteo kina uwezo wa kukamua tani 400 za miwa kwa saa na kuzalisha tani 170,000
za sukari kwa mwaka.
Kampuni ya Alteo inamiliki kiwanda cha sukari cha TPC
mkoani Kilimanjaro kwa ubia na Serikali ya Tanzania na kinazalisha tani 110,000 kwa mwaka.
Aidha, Waziri Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi wa
kiwanda hicho na kuwashawishi waongeze maeneo ya uwekezaji nchini.
“Tekonolojia
wanayoitumia katika uendeshaji wa kiwanda chao ni nzuri hivyo tumewashawishi
waje kuongeza maeneo ya uzalishaji wa sukari nchini ili tuweze kukidhi
mahitaji,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Tanzania kuna viwanda vitano vya
sukari ambavyo ni Mtibwa, Mahonda (Zanzibar), TPC, Kilombero na Kagera ambavyo
uzalisha tani 320,000 kwa mwaka wakati mahitaji ya ndani ya nchi kwa mwaka ni
tani 420,000.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar kuna
kiwanda kimoja cha sukari ambacho uzalishaji wake haukidhi mahitaji kutokana na
uhaba wa malighafi.
Dk. Khalid
amewakaribisha kampuni ya Alteo kwenda Zanzibar kushirikiana na Serikali katika
uwekezaji hususani kwenye viwanda vya sukari.
Naye Mtendaji
Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Patrick de Labauve amesema wamekubali kuongeza maeneo
ya uwekezaji wa mashamba ya miwa nchini.
Pia ameomba
Serikali iwapatie fursa ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Kilimanjaro
kwani kuna vivutio vingi vya utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro.
Akizungumzia kuhusu ajira amesema kiwanda cha TPC
kimeajiri wafanyakazi 3,000 wakiwemo 1,900 wa kudumu wa ndani utakaotosheleza
mahitaji na kupata ziada.
Kusimamia mfumo mzima wa usambazaji wa sukari nchini
ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wafanyabishara wenye tabia ya kuhodhi soko la
sukari kwa lengo la kusababisha upungufu usio halisi wa sukari (artificial
shortage).
Kuendelea kuhamasisha na kuweka mazingira mazuri ya
uwekezaji kwa wazalishaji wa sukari wa ndani ya nchi.
KIWANDA CHA
SAMAKI
Waziri Mkuu pia alitembelea kiwanda cha kusindika
samaki aina ya jodari na kuwakaribisha viongozi wa kiwanda hicho kuja nchini
kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya samaki.
Amesema Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji na
pia ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya samaki,
ambayo ni bahari, mito na maziwa ambayo aina mbalimbali za samaki.
Waziri Mkuu
amesema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha Mer des Mascareignes
kilichoko jijini Port Louis nchini
Mauritius.
“Tanzania kuna
fursa nyingi za uwekezaji hasa kutokana na mazingira yake. Mnaweza kuja
kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki tuna bahari, mito na maziwa
yenye samaki wa aina mbalimbali,” alisema.
Majaliwa alisema Serikali imedhamiria kuimarisha uchumi
wake kupitia sekta ya viwanda ili kuongeza tija kwa Taifa na kwa wananchi
kiujumla hivyo wanahitaji wawekezaji waliotayari kuja kuwekeza nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed alisema Tanzania
inahitaji wawekezaji watakaowekeza kwenye uvuvi wa kina kirefu na ujenzi wa
viwanda vya samaki.
Dk. Khalid alisema lengo la uwekezaji huo ni kukuza
uchumi wa Taifa pamoja kupanua soko la ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa
wananchi wake.
Naye Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Patrick Hill
alisema wamefurahia mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia fursa na
uwekezaji na kwamba wako tayari kushirikiana na Serikali.
Alisema kampuni yao inajishughulisha na usindikaji wa
samaki aina moja tu ya jodari na wananunua kutoka kwa makampuni makubwa ya
uvuvi huku wateja wao wakubwa wakiwa ni bara la Ulaya.
KIWANDA CHA NGUO
Akiwa kwenye
kiwanda cha nguo cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee kinachotengeneza
nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa nchini Mauritius chenye uwezo wa
kutengeneza tani milioni 40 hadi 50 kwa mwaka.
Waziri Mkuu aliwakaribisha wawekezaji hao kuja nchini
kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi na nguo kwa kuwa kuna malighafi
za kutosha kwa ajili ya uzalishaji huo.
“Tumefarijika na uwekezaji wenu na tumejionea namna
ambavyo mnavyoendesha kiwanda chenu kuanzia utengenezaji wa nyuzi hadi nguo,
hivyo tunahitaji viwanda kama hivi nchini Tanzania kwa sababu sisi tunazalisha
pamba nyingi na yenye ubora unaokubalika kimataifa,” alisema.
Waziri Mkuu alisema madhumuni ya kuwakaribisha
wawekezaji hao kuja Tanzania na kuwekeza katika
viwanda vya kutengeneza nyuzi yanalenga kuboresha kilimo cha pamba na
kuwawezesha wakulima kupata tija.
“Tunalima
pamba nzuri na hawa hawalimi wananunua kutoka nje ya nchi yao, hivyo wakija
kuwekeza Tanzania itawarahisishia kupata malighafi ya uhakika na kwa urahisi
” alisema.
Alisema
viwanda hivyo vitasaidia maendeleo ya kilimo cha pamba kwa sababu vitatoa ajira
kwa wananchi wengi hivyo kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
umasikini wa kipato.
Mbali na kuwakaribisha wawekezaji hao, Waziri Mkuu
alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuhakikisha wanajenga viwanda vya nyuzi
kwenye mikoa yote inayozalisha pamba ili waweze kuiongezea thamani kabla ya
kuiuza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa kiwanda hicho
David Too Sai Voon alisema wamefurahishwa na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili
ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya nyuzi na nguo.
David alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 1986 na
kwa sasa kimeajiri wafanyakazi 18,000 ambapo mauzo yao kwa ni dola milioni 200.
“Nguo tunazotengeza ni za kiwango cha kimataifa na tunauza katika maduka
makubwa barani Ulaya,”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.