WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi 19, 2017) kwa
ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa
kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur
Ramgoolam Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius
Mheshimiwa Vishnu Lutchmeenaraidoo.
Uzinduzi wa
jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo utawakutanisha
viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu
kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.
Pamoja na
kuhudhuria mkutano huo, pia Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary
Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara kati ya
Tanzania na Mauritius litakalofanyika Machi 23, 2017.
Aidha, Waziri
Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea maeneo maalumu ya
uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo.
Waziri Mkuu
ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt.
Khalid
Salum Mohammed
na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa . Charles Mwijage pamoja na
maofisa wengine wa Serikali.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.