Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi
Mwinyimvua akiongea na wafanyakazi wa ofisi hiyo (hawako pichani) wakati wa mkutano wa kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma uliofanyika leo jijini Dar es salaam tarehe 23 Juni, 2017.
Ofisi ya Waziri Mkuu imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia Juni 16-23 Barani Afrika,
kwa mwaka huu kauli mbiu ni
“Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utoaji Huduma: Vijana washirikishwe
kuleta Mabadiliko Barani Afrika”.
Kwa kuzingatia kauli mbiu hiyo yenye kujikita katika kushirikisha jamii katika utoaji huduma, Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi
Mwinyimvua amekutana na wafanyakazi wa ofisi hiyo leo jijini Dar es
salaam tarehe 23 Juni, 2017, ambapo wamejadili jinsi ya kuboresha
utoaji wa huduma kwa umma kwa kuzingatia weledi, uadilifu na ufanisi ili
kuhakikisha Dira na Dhima ya Ofisi hiyo inafikiwa.
Dira
ya Ofisi hiyo ni kutoa huduma kwa umma katika mazingira shindani ya
kiuchumi ili kuwa na maendeleo emdelevu, aidha Dhima ya ofisi hiyo ni
Kuratibu na kusimamia utoaji wa huduma zenye kuleta matokeo
yanaotarajiwa katika sekta zote ili kujenga mazingira ya kiuchumi kwa
maendeleo enndelevu.Ofisi
ya Waziri imekuwepo tangu mwaka 1962. Mwaka 1977, Ofisi ilipewa hadhi
yake kisheria kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambayo ilianzisha wadhifa wa Waziri mkuu. |
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.