Katibu
mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora ametembelea na kukagua kituo cha
operesheni ya mawasiliano ya dharura na kujua maendeleo ya kituo hicho
kilichopo Ofisi ya kanda Maalumu ya jeshi la Zima moto Jijini Dar es
salaam.
Akitoa
maelezo ya jinsi mradi huo unavyofanya kazi, Mratibu wa Taifa wa Mradi huo
Alfei Daniel, alisema Mradi huo unafuatilia dharura za maafa nchini ikiwemo
Ukame na Mafuriko umefadhiliwa na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani UNDP,
ambapo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za maafa na vyanzo vyake,
kuchambua taarifa hizo, kuhamasisha, kufuatilia, kutoa tahadhari za awali na
kuratibu dharura katika ngazi ya kitaifa.
Alfei alifafanua kwamba,
mradi huo una vituo 36 tofauti nchini ambavyo vina wawezesha kupata taarifa
popote walipo kupitia mtandao maalumu, unaosaidia kutoa tahadhari kwa wananchi
wa eneo linalotarajiwa kupata maafa, ambapo mpaka sasa mradi umechukua mabonde mawili
yaani bonde la Pangani na bonde la mto Ruvuma.
“Mfumo ambao umefungwa unaweza
kutabiri na kutoa taarifa za maafa zinazo weza kutokea popote katika vituo hivyo
kwa kutumia mtandao, kwa mfano kujaa kwa maji ambako kuna weza kupelekea mafuriko.
Mfumo huu ukikamilika utaweza kuonyesha ramani na vituo vyake vyote vya hali ya
hewa.” Alisema Alfei.
Aidha baada ya kupata maelezo
ya mradi huo Prof. Kamuzora alishauri mradi huo ufanye jitihada kutoa elimu ya uokoaji
kwa wanafunzi mashuleni na raia wote kwa ujumla, na kwa watu wasiokua na elimu ya
uokoaji watahadharishwe kukaa mbali na matukio ya maafa kwani wengi wao huathirika
au kupoteza maisha katika uokoaji kwa kukosa elimu hiyo.
“Ni lazima uongozi uhakikishe
matumizi mazuri ya rasilimali za mradi huu na kuzuia uharibifu wa vifaa na fedha
zinazotelewa na mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali kuendesha mradi huu”
Aliongeza Prof. Kamuzora.
Bw. Alfei alisisitiza kuwa mfumo
huo unasaidia sana TMA katika kutabiri mabadiliko ya hali ya hewa kwa uhakika wa
87%, Wizara ya maji wanaweza kupata data kwa ajili ya kukuza vyanzo vya maji,
vile vile hifadhi za taifa zinapata taarifa za hali ya hewa kwa urahisi kwa ajili
ya kuhabarisha watalii na kujua mienendo ya wanyama, kwa ujumla huu mfumo unasaidia
upatiknaji wa taarifa.
Mradi huu wa Uboreshaji wa Taarifa
za Mabadiliko ya Tabia nchi na Mifumo ya utolewaji wa tahadhari za awali ulianza
rasmi mwezi Januari, 2017 kwa dhumuni hasa la kuwezesha mawasiliano ya kujitahadhari
na maafa,kujiandaa na maafa, na kipindi cha maafa ambapo mawasialiana ya haraka
huitajika ili kuokoa maisha na makazi ya watu. Hivyo mradi huu umeundwa ili kuwezesha
mawasialiano ya saa 24 kwa siku saba za wiki.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.