NA.MWANDISHI
WETU
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Prof.Faustin Kamuzora
amewataka wakulima wa Wilaya ya Kasulu kulima kwa tija ili kuondokana na
changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa masoko.
Ametoa
kauli hiyo Novemba 08, 2018 alipofanya ziara katika maeneo ya Mradi wa
Kuboresha Mazingira ya Biashara Local
Investment Climate (LIC) ikiwemo Mradi
wa Umwagiliaji wa Tittye Wilayani Kasulu mkoani Kigoma ili kukagua na
kujiridhisha ubora na faida zitokanazo na mradi huo.
“Wakulima
wa Wilaya ya Kasulu hamna budi kubadili mitazamo katika uzalishaji kwa kuanza
kuweka mikakati ya kuzalisha kwa tija ili kuondokana na changamoto za kukosa masoko
ya mazao ikiwemo Mpunga na mihogo hivyo ni wakati muafaka kuwatumia maafisa
kilimo waliopo ili kupata mbinu mbadala za matumizi mazuri ya pembejeo za
kisasa ili kuzalisha kwa tija”.Alisema Prof.Kamuzora
Aliongezea
kuwa wakulima wanapaswa kuondokana na dhana potofu ya kilimo cha asili kinachohusisha
dhana ya kulima kwa dawa za kienyeji ambazo wamekuwa wakizitumia kwa muda mrefu
bila kuleta matunda wanayotarajiwa.
“Ni vyema
sasa kuachana na kilimo cha matumizi ya dawa za kienyeji na hatimaye muone
namna bora ya kuwatumia wataalam wa masuala ya kilimo ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na
teknolojia ili kuzalisha kwa tija.”Alisisitiza Prof.Kamuzora
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe.Kanali Simon Anange aliahidi kutekeleza maagizo
yaliyotolewa na Katibu Mkuu huyo pamoja na kutoa rai kwa wakulima wa Kasulu
kuendelea kuzalisha kwa tija ili kuendana na soko lililopo.
Aidha
alipongeza juhudi za Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa LIC kwa kuendelea
kuwawezesha wakulima wa wilaya yake kwa kuwapatia elimu na kuboresha
miundombinu ikiwemo ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji katika mashamba ya mpunga
ya Titye na kukiri ongezeko la uzalishaji toka mradi ulipoanza mwaka 2014 hadi
sasa.
“Mradi
wa umwagiliaji umekomboa wakulima 750 katika Wilaya yangu ya Kasulu hivyo,
niwatake sasa wakuliwa kuendelea kuutumia mradi huu wa kuboresha mazingira ya
biashara kwa kuhakikisha tunazalisha kwa tija pamoja na kushirikiana na sekta
binafsi”.alisisitiza Kanali Anange.
Kwa
upande wake mmoja wa wanufaika wa mradi
huu Bi.Evelyne Reuben alishukuru Serikali kwa jitihada za kuwafikia wakulima
kwa kutoa elimu ya kilimo cha kisasa pamoja na uboreshaji wa mazingira ya
kilimo na kuomba jitihada hizo ziendelee ili kumaliza changamoto za kukosekana
kwa masoko na kuiomba serikali kuendelea kuleta pembejeo za kilimo kwa wakati.
“Ninaipongeza
Serikali kwa kutukumbuka wana Kasulu ila ombi letu kama wakulima ni kupatiwa
pembejeo za kilimo kwa wakati pamoja na kuendelea kupewa elimu ya kilimo cha
kisasa ili kuwa na uzalishaji wenye tija zaidi”.Alieleza Evelyne.
=MWISHO=
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof.Faustin Kamuzora akuzungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika mradi wa Umwagiliaji wa Titye Wilayani Kasulu Kigoma. |
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.