NA MWANDISHI WETU
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amevipongeza Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa
kutoa maarifa mbadala kwa changamoto
zinazoikabili jamii. Hii inatoa hamasa kwa sababu wanaungana na sera za nchi katika
kuongeza fursa za kupata ajira.
“Mafunzo ya Elimu ya ufundi na
Mafunzo ya ufundi Stadi yanagusa eneo muhimu sana la vijana, vijana wengi
wamepata elimu hii kwa mafunzo ya muda mfupi miezi mitatu, miezi sita, miaka
mitatu ambayo yanawawezesha kupata ujuzi mbalimbali katika utendaji kazi pamoja na kutoa vyeti.”
Amesema hayo alipotembelea Maonesho ya Vyuo
vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi yanayofanyika Uwanja wa Jamhuri Mjini
Dodoma ambayo yamesaidia kutoa maarifa
kwa wananchi kujua fursa za ajira zilizopo katika maeneo yao, lakini pia kusaidia
wataalamu wetu kuwa na maarifa yanayoendana na soko la ajira linalohitajika
katika Nchi yetu
Naibu katibu mkuu Mmuya ametoa
rai kwa wanavyuo na wakufunzi kuendelea
kuangalia mahitaji ya jamii ili waweze kuandaa mafunzo ya muda mfupi ili kuweza kuwapatia wananchi ujuzi
unaotakiwa utakaosaidia kuzalisha ajira nyingi.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa
mitala na upimaji Dr. Annastelllah Sigweyo amesema baraza inaangalia program
zinazoanzisha zainaendana na uhitaji wa jamii baada ya kufanya utafiti wa eneo
husika na kwa kuzingatia ushauri wa wadau.
tunaangalia uwezo wa chuo
kinachotaka kutoa program kama kina uwezo wa kutoa ujuzi husika kwa kuangalia uwezo
wa walimu kitaaluma katika kutoa ujuzi, ndipo tunapopitisha mtaala kwa ajili ya
chuo husika.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.