Imeelezwa kuwa kundi
la vijana kati ya umri wa miaka 15 mpaka 24 wanaongoza kwa kuchangia maambikizi
mapya ya VVU – UKIMWI ambayo ni sawa na Asilimia 40 (40%).
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe.
Jenista Mhagama ameyasema hayo mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma alipokuwa
katika Mkutano na waandishi wa Habari uliyohusu maandalizi ya kilele cha maadhimisho
ya siku ya UKIMWI Duniani, yanayofanyika Disemba moja kila mwaka.
Akiongelea kuhusu
maadhimisho hayo yanayotarajiwa kafanyika kitaifa Mkoani Morogoro mwaka huu,
Waziri Mhagama alisema tafiti zilizopo zinaonesha kuwa kuna kila sababu ya
kuongeza nguvu kubwa kwa kundi la vijana ili kuliondoa kwenye uhatarishi wa
maambukizi ya vvu.
Aliendelea kusema kuwa
maadhimisho ya mwaka huu yatatoa kipaombele kwa kiasi cha cha kutosha kwa
vijana kushiriki kikamilifu kwenye majukwaa na matukio yaliyoandaliwa kwenye
maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka huu nchini kote kutokana na sababu
kwamba vijana ndo waingia kwenye maambukizi mapya kwa wingi.
“Tunapokwenda
huko mbele walau kwenye maadhimisho ya wiki ya kuelekea siku ya UKIMWI Duniani,
tutoe nafasi ya kuwasikiliza vijana kwa karibu zaidi wakongamane, wakutane na
viongozi wa dini na viongozi wa kimila, na wakati mwingine tumekuwa tukifikiri
kwamba labda, mienendo ya kimaadili kwa sasa imekuwa ikichagiza vijana wetu
kujikuta wanaingia kwenye kundi la maambukizi mapya kwa hivyo kwa kipindi hiki
kipaombele kitakuwa kwa kundi la vijana.” Alifafanua Waziri Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama
alisema kuwa zaidi ya mara tano tafiti zinaonesha kuwa wanawake wamekuwa na
uhiyari wa kupima ukilinganisha na wanaume; ambao hawajitokezi kupima na kuanza
matumizi ya dawa, hivyo kuna kila haja ya Serikali kupaza sauti juu kuwaomba
kina baba waingiwe na hali ya uhiyari katika kufanya maamuzi ya kupima.
Kwa Upande wake Makamu
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) Bw. Emmanuel
Reuben Msinga alisema kuwa kupitia Kliniki ya Huduma na Kinga (CTC) vijana
wanaweza kufikiwa kwa wingi na kupata hamasa ya kupima kwa hiyari, na vijana
wanahamasishana kukubali hali zao na namna ya kuwafikia vijana wingine ili
wakapime kwa hiayari.
Aliongeza kusema kuwa
NACOPHA ina kanda zake nchini na suala la uhamasishaji kwa sasa linafanyika
kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya na Mikoa.
Kauli Mbiu kwa
Maadhisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka huu inasema; “JAMII IONGOZE
KUTOKOMZEA UKIMWI.”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.