Wahitimu wa Chuo cha Biblia cha Evengelism Church wameaswa kuwa askari wazuri wa vita dhidi ya mmomonyoko wa maadili ambao unaendelea kushamiri katika jamii zetu hususani kwa vijana.
Wito
huo umetolewa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na
Uratibu) Mhe, Jenista Mhagama wakati wa
mahafali ya 83 ya chuo hicho yaliyofanyika, Sakila Katika wilaya ya Meru
Mkoani Arusha.
Waziri
aliwaambia wahitimu hao kwamba maendeleo ya taifa letu yanategemea sana nguvu
kazi na nidhamu ya kazi, japokuwa nchi yetu haiegemei
upande wowote katika maswala ya dini, lakini sehemu kubwa ya watu wake wanaamini
katika dini kupitia madhehebu mbalimbal
“ni muhimu mkawe mabalozi wazuri katika vita
hii na mkashirikiane na viongozi wengine wa dini na Serikali ili kwa pamoja
tuhakikishe tunalilinda taifa letu dhidi ya upotofu huu wa maadili”
alibainisha.
Aidha,
aliwasihi kuendelea kuliombea taifa amani, utulivu, upendo na mshikamano ili kulijenga
taifa.
Waziri
ametumia maandiko matakatifu, katika Injili ya Matayo (Sura ya 5:13-16) ambayo yalisema,
nami pia niwasihi popote mnapokwenda, mkawe chumvi ya dunia na kamwe msipoteze
ladha ya chumvi lakini pia mkawe mwanga wa ulimwengu ukaangaze mbele ya watu
ili wayaone matendo yenu mema wamtukuze baba yenu aliye mbinguni.
“Sina shaka kwamba,
wote mkitoka hapa mtakwenda kutekeleza jukumu la kichungaji na kufundisha watu
kwa upendo, uaminifu na kuwaongoza katika kweli maana huo ndio wito mlioitiwa,”
alifafanua
Kwa upande wake Dkt. Eliud
Issangya, Askofu Mkuu wa International Evengelism Church na Mkuu wa Chuo cha
Biblia Sakila; alisema wahitimu wa chuo cha Biblia wanapaswa kwenda kuweka mkazo wa kufundisha maadili
kwenye jamii.
“Msambaze maandiko kwa kulenga maadili na si
kwa kutafuta mali, bali watu waweze kuishi kwa kuthaminiana na wawe watu wenye
hekima,” alihimiza
Awali muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mhe, Joshua Nassari Mkuu wa wilaya ya Monduli alisema serikali ya mkoa wa Arusha
itaendelea kutoa ushirikiano wa kiroho kwa chuo hicho cha Biblia na madhehebu
mengine.
“Jamii yetu imekuwa ikipitia changamoto kubwa
za mabadiliko ya kimadili na kitamaduni hivyo tujikite katika kufundisha
maadili mema ya kitanzania na madili mema ya Imani ili tuwe na jamii
iliyostaarabika,”alihimiza
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.