KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi
amesema Serikali imefanya juhudi mbalimbali za Kisera, Sheria na Kimkakati ili
kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na Kati.
Dkt.
Yonazi aliyasema hayo katika kikao cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya
Biashara cha Baraza la Taifa la Biashara TNBC kilichofanyika jijini Dar es
salaam.
Alisema
Serikali imefanya jitihada za kukuza biashara nchini huku akizitaka sekta
binafsi kuendelea kushirikiana na serikali.
“Serikali
imefanya juhudi mbalimbali katika uwekezaji nchini ikiwemo mazingira ya
ufanyaji wa biashara ya kisera, kisheria na lengo ni kuhakikisha Tanzania
inakuwa kitovu cha biashara Afrika mashariki na kati.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill
Wanga alisema kikao hicho kimefanyika ili kujadili maendeleo ya biashara
nchini.
Alisema
kikao hicho kimejadili vivutio ambavyo serikali inaweza kufanya uwekezaji
zaidi katika sekta ya afya ili bima ya afya kwa wote itakapoanza iweze
kuwa na faida kwa Watanzania.
“Kikao
hichi ni muendelezo wa vikao ambavyo tumekuwa tukifanya mara kwa mara katika
kujadili maendeleo ya biashara ambapo katika kikao hiki kimejadili kuhusu
miundombinu ya mtandao katika katika nchi yetu.
Aliongeza
kuwa :”Tumekubaliana kufanya utafiti kuhusu madhara ya vita katika mashariki ya
kati katika uchumi wetu.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.