Thursday, December 7, 2017

MAJALIWA ATEMBELEA UWANJA WA JAMHURI DODOMA KUKAGUA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA UHURU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia)  kuhusu maandalizi ya Uwanja wa Jamhuri wa mjini Dodoma kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru. Mheshimiwa Majaliwa alikagua uwanja huo Desemba 7, 2017.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia)  kuhusu maandalizi ya Uwanja wa Jamhuri wa mjini Dodoma kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru. Mheshimiwa Majaliwa alikagua uwanja huo Desemba 7, 2017.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua maandalizi ya sherehe za miaka 56 ya Uhuru na kusema kuwa ameridhishwa na hatua zilizofikiwa.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamsi, Desemba 7, 2017) baada ya kupokea taarifa ya kamati ya maandalizi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

Waziri Mkuu alisema Kamati ya Kitaifa na Kamati ya Mkoa zimejipaga vizuri na pia akagusia kuridhishwa kwake na hatua ya kamati hizo kuwaalika wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Aliwataka wanakamati hao wanahakikishe wanasimamia vizuri mapokezi ya wageni na wanazingatia ratiba. “Wananchi wakija uwanjani wakaguliwe mapema na kuingizwa uwanjani ili kuepuka usumbufu wa kukaa kwenye foleni kwa muda mreru,” alisema.

Mapema, akitoa taarifa ya maadalizi hayo, Waziri wa Nchi (OWM) anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Bibi Jenista Mhagama alisema mbali ya gwaride la heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu, kutakuwa pia na maonesho ya halaiki ya chipukizi wa shule za sekondari za Dodoma, kwaya maalumu kutoka Kyela, wimbo maalum ulioandaliwa na wasanii wa kizazi kipya na vikundi vya ngoma kutoka Kigoma, Ruvuma na Zanzibar.

“Tutakuwa pia na onesho la makomandoo kuruka kutoka kwenye helikopta, ndege za kijeshi, gwaride la mkoloni, kwata la kimyakimya na onesho la askari wa usalama barabarani,” alisema.





EmoticonEmoticon

Note: Only a member of this blog may post a comment.