WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya NMB kwa kuchangia huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo elimu, afya na michezo.
Ametoa pongezi hizo leo (Jumatano, Mei 30, 2018) wakati akizungumza Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker ofisini kwake Magogoni jijini Dra es Salaam.
Amesema katika jitihada za Serikali za kufufua ushirika na hasa kwenye mazao makuu matano, wakulima wamehamasishwa wafungue akaunti ili malipo ya fedha zao yafanywe moja kwa moja kweye akaunti zao.
“Tumehamasisha wakulima wote wafungue akaunti ili malipo ya mazao yao yafanywe mojamoja katika akaunti zao jambo ambalo litaepusha wizi au kunyang’anywa fedha wawapo mitaani, na kupitia mawakala walioko vijijini, wataweza kupokea fedha hizo,” amesema.
Amesema uwepo wa mawakala wa benki hadi vijijini, umesaidia kuwafanya Watanzania wasiweke fedha ndani ya nyumba zao.
Akizungumzia mchango wa Benki hiyo kwenye huduma za jamii, Waziri Mkuu amesema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuchangia vitabu, madawati na michezo ambapo imetoa mchango wa sh.milioni kwa timu ya soka ya Namungo iliyoko wilayani Ruangwa.
“Tumeona Benki ya NMB ikifadhili timu mbalimbali za ligi kuu kama vile AZAM, na sasa wameanza kuchangia timu za daraja la kwanza kwa kuichangia timu ya Namungo shilingi milioni 10. Pia walichangia sh.milioni kwenye ujenzi wa uwanja wa kisasa kule Ruangwa, tunawashukuru sana,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Bussemaker alisema wamefurahi kupata fursa ya kuichangia timu ya Namungo na kwamba wataifuatilia kwa karibu kuona ushiriki wake ukoje kwenye ligi hiyo. “Pia tunaitakia kila la kheri kwenye ushiriki wao wa ligi daraja la kwanza,” alisema.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.