NA.MWANDISHI
WETU
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah
Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania, Sarah Cooke mapema hii leo Machi 13, 2019 katika ofisi zake
Jijini Dodoma
Lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kujadili
maeneo muhimu yanayohusu masuala ya
uwekezaji ambapo Waziri Kairuki alieleza vipaumbele muhimu vya uwekezaji vitakavyochangia adhma ya Serikali ya kuwa na
uchumi wa viwanda ikiwemo kuwekeza katika maeneo ya kilimo, elimu, afya, viwanda
vya nguo pamoja na ujenzi wa Miundombinu ya barabara.
“Ninafarijika kwa ujio wako na ni ishara
nzuri ya mahusiano mazuri yaliyopo baina
ya nchi hizi mbili naamini yatasaidia katika fursa za uwekezaji hasa kwa namna
Uingereza ilivyochangia katika maeneo muhimu nchini ikiwemo elimu,”alisema
Kairuki
Waziri aliongezea kuwa, Serikali itaendelea
kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kwa kuzingatia mchango unaotokana na wawekezaji hasa katika kukuza uchumi na
kuleta maendeleo nchini.
Waziri Kairuki alieleza kuwa, kuwepo kwa
Idara ya uwekezaji katika Ofisi ya Waziri Mkuu ni hatua muhimu kwani itasaidia
kuongeza nguvu ya ufuatiliaji na utekelezaji wa masuala hayo na kuendelea kuleta
mabadiliko katika kutatua changamoto zilizozikabili sekta hiyo.
Aidha alimshukuru balozi huyo kwa hatua ya
mazungumzo yenye tija pamoja na kuendelea kuunga mkono nchi ya Tanzania na
kuwataka kuendeleza urafiki huo kwa kuwekeza zaidi katika maeneo aliyoyaainisha
ikiweko yale ya vipaumbele.
Naye Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Sarah
Cooke aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na sera zinazovutia wawekezaji
pamoja na maboresho yanayofanywa kuwavutia wawekezaji nchini ikiwemo maeneo ya
ulipaji wa kodi.
“Tunaelewa kuwa Serikali inafanya jitihada
kubwa katika kuboresha mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja na mazingira ya
ulipaji wa kodi tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuwa na mchango katika
maendeleo ya nchi pamoja na kuimarisha mahusiano yaliyopo,”alisisitiza Cooke.
=MWISHO=
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.