Na.
OWM, MWANZA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
John Mongella amebainisha kuwa takribani ajali za majini zaidi ya mia tatu huripotiwa kuwa zimetokea
mkoani humo. Ajali hizo ni zile ambazo huripotiwa rasmi tu katika mamlaka husika , aidha inasadikika zipo
ajali nyingi ambazo hutokea lakini huwa haziripitiwi kutokana na jiografia ya mkoa huo. Mkoa wa
Mwanza una visiwa zaidi ya 162 ambapo kati ya Visiwa hivyo vipo ambavyo watu
wanayo makazi ya kudumu na vingine watu huishi kwa muda mfupi.
Akiongea wakati akifungua Mafunzo kwa Kamati ya Usimamizi
wa maafa ya mkoa huo, yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara
ya Uratibu wa shughulii za maafa Leo, tarehe 17 Aprili, 2019, jiijini Mwanza,
Mongella amefafanua kuwa ajali za vyombo vya usafiri hasa vya majini zinaweza
kupunguzwa sana kama wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivyo watazingatia
sheria na Kanuni zinazotawala uendeshaji
wa vyombo hivyo.
“Suala muhimu la Kuzingatia
ni kuhakikisha mamlaka zetu za serikali za mitaa zinaimarisha utawala bora
unaotoa nafasi kwa jamii kushiriki
katika kuzuia na Kupunguza madhara ya majanga, kujiandaa, kukabili na kurejesha
hali baada ya maafa kutokea ikiwa ni pamoja na kutoa elimu, taarifa za
tahadhari ya awali kwa wakati muafaka na kuandaa rasilimali zinazohiotajika ,
Ni wajibu wetu kuhakikisha sheria zinasimamiwa kikamilifu ili kuepuka maafa“
alisisitiza Mongella.
Naye Mkurugenzi wa Uratibu
wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, ameitaka
Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya mkoa huo
kuandaa Mkakati wa Kupunguza madhara ya maafa pamoja na Mpango wa kujiandaa na
kukabili maafa, Aidha, ameeleza kuwa Ofisi
ya waziri Mkuu imeendesha mafunzo hayo ili kuijengea uwezo kamati hiyo ambayo ni
chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathimini na kutekeleza masuala
ya kitaalam kuhusu usimamizi wa maafa, kuzuia na kupunguza madhara ya majanga
ya aina zote katika mkoa.
“Upunguzaji wa madhara ya
maafa ni suala mtambuka linalohusika katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi
na kijamii sekta zote. Suala la usimamizi wa maafa linahitaji utashi wa kisiasa
na kuwajibika kitaalam, kisheria, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi, mipango
makini ya maendeleo, ufanisi wa utekelezaji wa sera, mifumo ya tahadhari
inayojibu matakwa ya jamii” alisema
Kanali., Matamwe.
Mwaka jana, Mwezi
Septemba, mkoa wa Mwanza ulipata maafa makubwa baada ya Kivuko cha MV. Nyerere
kuzama na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200 na wengine 40 waliokolewa.
Kufuatia maafa hayo Mkoa huo umeendelea na jitihada za kuzijengea uwezo kamati
za Usimamizi wa Maafa za mkoa huo
Mafunzo hayo
yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa shughuli za maafa,
yamehudhuriwa na wajumbe wote wa Kamati ya Usimamizi wa maafa kwa kuzingatia
Kifungu cha 13 cha sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 7 ya mwaka 2015.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.