Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista mhagama amewataka waajiri wote
nchini kutonyanyasa wanawake katika masuala ya kazi ili kuwa na usawa maeneo ya
kazi.
Ameitoa
kauli hiyo hii leo tarehe 30 Aprili, 2019 alipokuwa akifungua semina ya siku
moja ya viongozi wanawake kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini
walipokutana kujadili masuala yanayowahusu wawapo kazini ikiwemo; haki na
wajibu wao wawapo kazini iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Paradise Inn Jijini Mbeya.
Waziri
alieleza kuwa waajiri hawana budi kubadili mitazamo hasi iliyopo katika jamii
ya kuona wanawake ni viumbe dhaifu na wenye majukumu mengi yanayoweza kukwamishi
jitihada zao wawapo kazini badala yake wawaone kuwa ni viungo muhimu katika
kuchangia uzalishaji na maendeleo nchini.
“Mchango
wa wanawake ni mkubwa endapo utatambuliwa na kuthamini katika nyanja zote za
ukuaji wa uchumi, hivyo ni vyema maeneo ya kazi waajiri watimize wajibu wao kwa
kundi hili kwa kuzinigatia sheria zilizopo na wasinyanyaswe na waendelee
kuheshimiwa na kupewa haki na stahiki zao kama wafanyakazi wengine.”alisisitiza
Waziri Mhagama.
Waziri
alieleza jitihada za serikali ni kuhakikisha inasimamia vyema sheria na
taratibu za kazi nchini kwa kuliangalia kundi hili ili kuwa na waajiriwa wenye
kuzingatia usawa wa kijinsia.
“Ninakemea
vitendo vya unyanyasaji wa haki za wanawake kazini ikiwemo kukoseshwa haki zao
na vyama hivi vya wafanyakazi viendelee kuleta tija katika kukemea matendo
hayo,”alisistiza Waziri Mhagama.
Aidha
Waziri aliwataka wanawake kuendelea kuvitumia vyama vya wafanyakazi kama jukwaa
maalum la kueleza na kutatua changamoto zao.
Aliongezea
kuwa, pamoja na changamoto wanazokutana nazo wanawake hawana budi kujiendeleza
kielimu ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo katika masuala
ya kazi.
“Wanawake
umefika wakati kuendelea kujiendeleza katika eneo la elimu ili kuwa na vigezo
mahususi vitakavyo wapa nafasi nzuri katika maeneo yenu ya kazi.”alisisema Waziri
Mhagma.
Naye
rais wa Shirikizo la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya
alimpongeza waziri pamoja na changamoto zilizopo katika kufikia haki sawa kwa
wote , alieelza umuhimu wa kuendelea kuliinua kundi hili ili kuwasaidia
wanawake wa Kitanzania katika kupata haki na usawa kwenye maeneo yao ya kazi.
“Wanawake
wana uwezo mkubwa hivyo tuendelee kujali na kutunza nafasi zao wawapo kazini
ili kuwezesha Taifa kuendelea kuwa na maendeleleo,” alisisitiza Nyamhokya.
Kwa
upande wake Mwenyekiti Kamati ya Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Bi. Rehema Ludanga alieleza kuwa, ni wakati sahihi kuendelea kuchangamkia fursa
za maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vya wanawake vitakavyosaidia
kuondokana na hali ya utegemezi na kuchangia katika ongezeko la uzalishaji
nchini.
Rais wa Shirikizo la Vyama
vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akisalimia washiriki wa semina
hiyo.
|
Katibu Mkuu wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Dkt. Yahya Msingwa akieleza jambo wakati wa
semina hiyo.
|
Mwenyekiti Kamati ya
Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bi. Rehema Ludanga
akichangia jambo wakati wa semina hiyo.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista mhagama (katikati) pamoja na viongozi wa Vyama vya wafanyakazi
nchini, wakifuatilia hoja wakati wa semina maalum kwa wanawake kutoka katika
vyama mbalimbali vya wafanyakazi nchini iliyofanyika Aprili 30, 2019 Jijini
Mbeya.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista mhagama pamoja na baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo
wa umoja na mshikamano wakati wa semina hiyo.
|
Washiriki wa semina hiyo
wakiimba wimbo wa kumshukuru mgeni rasmi kwa kujumuika nao katika semina hiyo.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista mhagama (katikati walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya washiriki wa semina hiyo mara baada ya ufunguzi rasmi Aprili 30, 2019 Mkoani
Mbeya.
|
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.