Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista mhagama amewaasa wafanyakazi nchini kufanya kazi kwa bidii
na uzalendo ili kuendelea kutimiza wajibu wao na kujiletea maendeleo nchini.
Ametoa kauli hiyo mapema
hii leo Aprili 29, 2019 alipokuwa akihutubia wafanyakazi walioshiriki katika
semina maaalum ya wafanyakazi iliyowakutanisha wajumbe kutoka vyama mbali mbali
vya wafanyakazi ili kujadili chimbuko la sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) na
kujadili masuala ya sheria za kazi katika ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.
Akizungumza na wajumbe wa
semina hiyo, waziri Mhagama aliwaasa wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa
weledi na tija ili kuendelea kuwa na taifa lenye maendeleo kwa kuzingatia
mchango wa wafanyakazi nchini.
“Wafanyakazi endeleeni
kufanya kazi kwa umoja, weledi huku mkizingatia kanuni, taratibu na sheria
zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yenu pasipo kukiuka masuala ya msingi
yanayowahusu,”alisema Waziri Mhagama.
Aliongezea kuwa, katika
kuhakikisha Taifa linakuwa na maendeleo endelevu ni vyema wafanyakazi
wakaendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuzingatia mchango mkubwa
wa wafanyakazi nchini katika kujiletea maendeleo kwa kuzingatia tija
walioyonayo nchini.
“Niwakumbushe kuwa nyie ni wadau
muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu na Serikali inawategemea katika kuchangia
maendeleo ya nchi hivyo mnapaswa kujali maeneo yenu ya kazi na kuendelea
kuvitumia vyama vya wafanyakazi katika kueleza masuala yenu na kutumia vyama
vyenu kutatua changamoto zinazowakabili,”alisisitiza Waziri Mhagama
Sambamba na hilo Waziri
aliwataka wafanyazkai kuendelea kuzingatia uwajibikaji wenye misingi ya haki na
usawa ili kuwa na mazingira salama ya kiutendaji pasipo kuvunja sheria za
wafanyakazi ili kuwa na matokeo chanya kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa TUICO Taifa Bw. Paulo Sangeze alieleza shukrani zake kwa namna serikali
inavyoendelea kuunga mkono uwepo wa Vyama vya wafanyakazi na kuahidi kutoa
ushiorikiano kila itakapohitajika.
“Kwa dhati ya moyo wangu na
kwa niaba ya TUCTA ninatoa shukrani kwa Serikali kwa namna inavyounga mkono
shughuli za vyama vya wafanyakazi na hakika kumekuwa na mabadiliko makbwa tofauti
na ilivyokuwa awali,”alisisitiza bw. Sangeze
Sehemu ya wajumbe
walioshiriki semina hiyo wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano.
|
Mwenyekiti wa TUICO Taifa
Bw. Paulo Sangeze akitoa neno la shukran kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina.
|
Mwenyekiti Kamati ya
Wanawake Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Bi. Rehema Ludanga akichangia
jambo wakati wa semina hiyo.
|
Sehemu ya wajumbe
walioshiriki semina hiyo wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano.
|
Sehemu ya wajumbe wa semina
hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista
Mhagama (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.
|
Rais wa Shirikisho la Vyama
vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akichangiua jambo wakati wa
semina hiyo.
|
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.