Na
Mwandishi wetu- Pwani
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya amehimiza Ofisi za Umma na Ofisi Binafsi kuweka
anuani za makazi katika majengo ya Ofisi zao ili kuwa mfano kwa wananchi
wengine. Anuani hizo zitasadia kuonesha jina la Ofisi yenyewe Mtaa iliyopo na
eneo ambalo posti kodi hiyo ipo.
Naibu katibu Mkuu Mmuya
amesema hayo katika ziara yake Mkoani Pwani tarehe 13 /05/2022 alipotembelea na
kupokea taarifa ya Mkoa ya utekelezaji wa Anuani za makazi. Kwa sasa ngazi ya Taifa
tumefikia 90% ya matarajio yetu lakini tunazidiana Mkoa na Mkoa.
Amepongeza Mkoa wa Pwani kwa
kutekeleza vyema zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na kufuata miongozo
iliyowekwa katika utekelezaji wa anuani za makazi. “Ziara imelenga kujionea
uhalisia ili mwezi huu, tutumie kurekebisha dosari chache tulizogundua kwa
kupokea taarifa kwenye mfumo au kwa ziara mbalimbali tunazozifanya au taarifa
tunazopatiwa alisema, Naibu Katibu Mkuu Mmuya”
“zoezi la anuani ya makazi ni
endelevu, kila mmiliki mwenye eneo ambalo limejengwa au halijajengwa anapaswa
kuwa na namba,alisema Naibu Katibu Mmuya”. Hiyo itasaidia kujua mahali eneo
lilipo, wananchi wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya umuhimu wa zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na itaongeza
dhana ushirikishwaji wa wananchi.
Akihitimisha Kaimu Injinia wa
Tanroad Mkoa wa Pwani Meneja Heririsper Mollel amesema utekelezaji wa anuani za
makazi umefika katika hatua nzuri ukamilishaji wake kwa sasa wamejikita katika
kurekebisha vibao vilivyokosewa.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.