Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya ameshauri watendaji kuanza
kutumia taarifa za mfumo wa Anwani za makazi Postikodi kwenye barua za ofisi ili
kurahisha mawasiliano kwa watu kujua eneo zinapopatikana Ofisi
“Watendaji tuanze
kujitambulisha kwenye mikutano kwa mfumo wa Anwani za makazi ili kutoa hamasa
zaidi kwa wananchi alisema Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na
Uratibu”
Naibu Katibu Ofisi ya waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu ametoa ushauri huo
Katika ziara yake ya kikazi Mkoani Pwani Halmashauri ya Kibaha Mji,
alipoenda kujionea utekelezaji wa Operesheni Anwani za makazi.
Afisa Mtendaji mtaa wa mkoani
A Kibaha Bwn. Jakson Mwakalima amesema tayari wameshapata mtengenezaji wa vibao
vya nyumba, ambavyo mwananchi anaenda kununua kwa shilingi elfu Mbili na
kubandika kwenye nyumba yake.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.