Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza
wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa
ajili ya maendeleo yetu wenyewe.
“Unapohesabiwa unakuwa upo
katika mpango wako wa maendeleo, katika sehemu yako unayoishi na Nchi kwa
ujumla”
Hayo yamesemwa na waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene baada
ya kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi jimboni kwake Kibakwe katika
Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Amefafanua kwamba
usipohesabiwa, unakosa lile fungu lako katika miaka 10 ijayo kwa ajili ya
mipango ya maendeleo.
“Bado tuna siku tano mbele kwa
ajili ya kuhesabiwa hakikisha umeacha kumbukumbu za watu walilolala usiku wa
kuamkia tarehe 23 Agusti 2022, alisema Waziri”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.