Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema Mzee William Kusila alipenda kuona viongozi wanazingatia miiko, na kuishi kwa kuwa mfano mwema kwa jamii.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene
alipokuwa akitoa salamu za serikali katika ibada ya mazishi ya Mzee Williamu
Jonathan Kusila aliyezaliwa Mwaka 28/02/1944 na kufariki 21/08/2022, iliyofanyika nyumba kwake kata ya Mtitaa-Bahi
Dodoma 26/August/2022.
“Mzee kusila ni kipimo cha mtu
muadilifu; mtu mwenye Upendo, na mtu aliyefanya mambo mengi mazuri ambayo
tunapaswa kuyaiga na kuyaenzi.”
Tumepoteza kiongozi wa kisiasa
aliyeshika nafasi mbalimbali za umma na kutimiza majukumu yake ipasavyo, ni mtu
aliyepinga na kukataa rushwa, alisema Waziri.
Aidha ametoa rai kwa Watoto wa
Mzee Kusila kuzidi kushirikiana na kushikamana ili kutunza jina na heshima ya baba.
“Amefafanua watu hawazaliwi
sawa, mtatofautiana kwa uwezo wa elimu, uwezo wa kipato na mambo mengine lakini
wote ni Watoto wa mzee Kusila ni lazima mtengeneze mamlaka itakayosaidia
kuwaongoza kama familia”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary
Senyamule amesema Mzee William Kusila alikuwa
Mkuu wa Mkoa wa Saba wa Dodoma kati ya Mwaka (1993-19995) alikuwa Mbunge wa
jimbo la Bahi na katika vipindi tofauti amekuwa waziri wa kilimo, Waziri wa
Mawasiliano na Uchukuzi na amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa
wa Dodoma.
“Alifanya kazi kwa upendo Mkubwa; aliokuwa nao
kwa wananchi wa Dodoma, Baba yetu aliongoza kwa Vitendo na sio kwa kuagiza,
kama alisema limeni nayeye alikuwa analima”
Naye Mbunge Mstaafu wa jimbo
la Chilowa Mhe. Hezekiah Chibulunje akitoa salamu za rambirambi amesema
anamkumbuka mzee Kusila kwa jitihada zake za kuondoa Njaa Dodoma na kuhakikisha
tunapanda mazao yanayostahimili ukame.
“Alikuwa na uchungu sana
katika kuondoa njaa na vile vile katika swala la zima la kusimamia elimu,
nimefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa sana bila nongwa”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.