Serikali imetoa rai kwa wadau
wa kilimo kuendelea kutambua Ubunifu na Teknolojia mpya zinazooneshwa katika
maonesho ya Nanenane ili kuweza kuzikuza na kuzisambaza kwa walengwa wakiwemo
Wakulima, Wafugaji na Wavuvi
“Maonesho ya Nanenane yawe ni
kitovu cha teknolojia mpya (innovation hub) kwa kuhakikisha kuwa wadau wote wa
Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi wanashiriki Maonesho haya, ili kuonesha na
kujifunza teknolojia zote zinazotoa majawabu ya changamoto za Sekta hizo,”
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene
alipokuwa akihutubia katika kilele cha maonesho ya siku ya Nanenane kanda ya
Mashariki yaliyofanyika Uwanja wa Mwl. Julius Nyerere Mjini Morogoro kwa niaba
ya mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa
Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Sote tunatambua mchango mkubwa
wa Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika kuchangia pato la Taifa, ajira,
usalama wa chakula na malighafi za viwandani. Ndiyo maana kauli mbiu ya
maonesho ya mwaka huu inasema “Ajenda ya Kilimo ni Biashara, Shiriki
Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
“Waoneshaji wanatakiwa
kuhakikisha kuwa takwimu na taarifa sahihi zenye ulinganifu kuhusu teknolojia
na bidhaa wanazoonesha zinakuwepo ili ziweze kuwasaidia walengwa kufanya
maamuzi sahihi, alisema Waziri”
Aidha Maonesho ya Nanenane
yatumike kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta za Kilimo, Mifugo
na Uvuvi ili kuvutia wawekezaji wengi.
Amefafanua kila ngazi kwa
maana ya Kanda, Mikoa, Halmashauri na Wadau wengine ifanye tathmini kwa
kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo hali ya ushiriki na uhalisia wa teknolojia
zinazooneshwa kama zinatumika katika maeneo wanayotoka.
Naye naibu waziri wa kilimo
Mhe. Anthony Mavunde amesema bajeti ya kilimo imetoka billioni 294 (2021-2022)
mpaka kufikia billioni 954 kwa mwaka wa fedha (2022-2023). Wizara ya kilimo
tumejipanga kuleta mapinduzi ya kweli katika kufikia ajenda ya 2030 kwa
ushirikiano wa wadau wote kuikuza sekta ya kilimo kufikia 10%.
“Bajeti ya umwagiliaji
imepanda kutoka billioni 46 ya mwaka wa fedha uliopita hadi kufikia billioni
zaidi ya 400 kwa mwaka huu wa fedha (2022-2023). Mikakati ni kuwa na
mfumo mzuri wa Umwagiliaji na utekelezaji wake umeanza kwa kupitia mabonde yote
22 ya umwagiliaji ili kufanya upembuzi yakinifu na usanifu ili tuanze kufanya
kilimo cha umwagiliaji katika maeneo hayo, alisema Naibu waziri.”
Amebainisha katika Utafiti
bajeti imepanda kutoka billioni 11.7 kwenda billioni 40 ili kuviwezesha vituo
vya utafiti kuja na mbegu bora na mbegu ambazo zinastahimili ukame, sambamba na
kujengea uwezo vituo vyetu hasa katika maabara za kupima afya ya udongo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Mhe. Fatma A. Mwasa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha pembejeo kwa wakulima. Kupitia ruzuku hiyo
mkulima hata nunua kwa bei ya kawaida bali kutakuwa na punguzo ili kumuwezesha
mkulima azalishe kwa tija.
“Maonesho haya yana umuhimu
mkubwa na yanatoa elimu kubwa kwa wakulima, tumedhamiria kuichukua teknolojia
tuliyoipata kuihamishia vijijini alisema mkuu wa mkoa wa Morogoro.”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.