Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu
Dkt. Jim Yonazi amewaasa wanaume kuwa mstari wa mbele katika kushiriki masuala
ya lishe kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wanawake ili kuwa na taifa
lenye lisha bora kuanzia ngazi ya familia.
Ameyasema
hayo wakati akizungumza na wanakijiji wa Mpandapanda katika Kata ya Kiwira
Wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya katika kuadhimisha Siku ya afya na Lishe ngazi
ya kijiji ambapo iliadhimishwa kijijini hapo.
Katibu
Mkuu Dkt. Yonazi amesema kuwa wanaume wamekuwa mstari wa nyuma katika
utekelezaji wa afua za lishe hivyo kukwamisha jitihada zinazofanywa na
wakinamama katika kuhakikisha watoto wanapata lishe bora.
“Niwaombe
wanaume wote kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa na
lishe bora kwa kushirikiana pamoja tutakuwa na watoto wenye afya bora na kuwa
na Taifa lenye Lishe bora ili kuchochea maendeleo yetu,” Alisema
Akieleza
kuhusu jukumu la ofisi yake amesema, itaendelea kuratibu masuala ya lishe
nchini kwa kushirikia na wadau kwa kuzingatia miongozo iliyopo.
“Ofisi
ya Waziri Mkuu imeendelea kuratibu shughuli za Serikali na kuhakikisha miongozo
ya masuala ya lishe inatekelezwa ipasavyo ili kila mmoja kujua majukumu yake na
kuwa na nia thabiti katika utekelezaji wa masuala ya lishe nchini,” Alisisitiza
Dkt. Yonazi
Kwa
uapnde wake Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Masuala ya Lishe
Bi. Afshan Khan alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhakikisha Taifa
linakuwa na afya bora kwa kuwa na mikakkati inayotekelezeka.
“Tuna
ahidi kuendelea kutoa ushirikino wa kila hali kwa kuhakikisha tunaboresha afua
za lishe, ninaipongezea Tanzania kwa kuwa na rasilimali zote muhimu, huku
nikiupongeza mkoa wa mbeya kwa kuwa na vyakula bora na muhimu kwa afya zetu
niwasihii endeleeni kula vyakula vyenye virutubisho kwa kuzingatia mazingira
yenu yanaruhusu, yatumieni katika kuimarisha afya kwa kila rika,” alisema Khan
.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Ben Malisa akitoa salamu za mkoa kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa huo alisema mkoa umeendelea kutekeleza masuala ya lishe
kwa kuhakikisha inatatua changamoto za masuala hayo ikiwemo ya udumavu na
utapiamlo ambapo alisema ajenda ya lishe imeendelea kupewa kipaumbele mkoani
humo.
“Hali ya Lishe kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano
imeendelea kuimarika kutokana na juhudi kubwa za utoaji wa elimu ya Lishe
katika jamii. Kiwango cha watoto wa umri chini ya miezi sita walionyonyeshwa
maziwa ya mama pekee kimeongezeka kutoka asilimia 27.3 mwaka 2014 hadi asilimia
71 mwaka 2018,”alisema Ben Malisa
Alibainisha kuwa takwimu zinaonesha kwa mwaka 2022 hali
ya Lishe imeimarika ikilinganishwa na mwaka 2018 ambapo kiwango cha udumavu
katika Mkoa wa Mbeya kimepungua kutoka asilimia 33.8 hadi 31.5 ingawa kiwango
hiki bado kipo juu ya kiwango cha Kitaifa ambacho ni asilimia 30.
Aidha, kiwango cha uzito pungufu kimepungua kutoka
asilimia 9.8 hadi 1.4, ukondefu umepungua kutoka asilimia 2.7 hadi 0.6 na uzito
uliozidi umepungua kutoka asilimia 5.3 hadi 5.2.
Aliongezea
kuwa Juhudi kubwa zimefanyika katika kipindi cha miaka kumi ili kuboresha
Afua za Lishe katika Mkoa kupunguza kiwango cha udumavu na aina nyingine zote
za utapiamlo. Afua shirikishi za Lishe zinazolenga siku 1000 za mwanzo wa
maisha ya mtoto kuhakikisha athari ya muda mrefu katika Lishe, ukuaji na
maendeleo ya watoto zinatekelezwa kulingana na Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa
Lishe wa Sekta Mbalimbali (NMNAP II, 2022-26).
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.