Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshugulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt Jim Yonazi amesema, mfumo
wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Shughuli za Serikali ni mfumo
mahususi wa uboreshaji wa utendaji Serikalini kwa lengo la kuona ni namna gani Rasilimali
za Serikali zinaboreshwa na Kutumika vizuri.
Hayo ameyasema Mapema leo
Ofisini kwake Jijini Dodoma alipokuwa katika mahojiano maalum na chombo kimoja
cha Habari, katika kuelekea Kongamano la wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na
Tathmini litakalofanyika Jijini Arusha Wiki Ijayo, ambapo Dkt. Yonazi ameeleza
kuwa, Uratibu wa Shughuli za Utendaji wa Serikali katika eneo la Ufuatiliaji na
Tathmini una nia ya kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya Serikali unafanikiwa
na malengo yanafikiwa.
Aliendelea kusema kuwa Dhana
hii, ni dhana ambayo inalenga katika kuangalia utekelezaji wa Miradi ya Serikali
Nchi nzima na kuona kama malengo yaliyowekwa katika Miradi hiyo yanafanikiwa. “Ili
malengo hayo yaweze kufanikiwa ni lazima tufanye Ufuatiliaji tujue nini
kinaendelea, tufanye Tathmini dhidi ya ile mipango ambayo ilikuwa imewekwa,
lakini vilevile tuangalie kwamba tunajifunza nini kutokana na kile ambacho
tumekiona kutoka katika Ufuatiliaji na Tathmini,” Alifafanua.
Aidha, Dkt. Yonazi Alimshukuru
Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuja
na wazo la kuanzisha mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini Nchi nzima,na kuweka vitengo
na Idara mahususi kwa ajili ya kazi hiyo katika Wizara na Taasisi za Serikali kwa
lengo la kuzipa uzito mkubwa ripoti zinazotokana na Ufuatiliaji na Tathmini
katika maamuzi, mijadala na mipango ya Serilikali ili kufikia malengo tarajiwa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na
Uratibu Bi. Sakina Mwinyimkuu amesema pamoja
na kongamano hilo kuhusisha wataalam na wadau mbalimbali nchini na nje ya nchi,
wananchi kwa Ujumla wanaalikwa kupata fursa ya kufahamu namna ambayo serikalini
inatekeleza miradi kwani kwa kiasi kikubwa miradi mingi inakwenda kwa wananchi “Mwananchi
ndiyo mdau wa kwanza kwani yeye ndo anaweza kujua mradi flani unatekelezwa
vizuri katika eneo husika, kwa hivyo tunaona pia ni fursa kwa mwananchi kuweza
kufahamu na kutoa hali halisi ya utekelezaji wa miradi katika maeneo yao.”
Alisisitiza.
Kongamano hilo la Pili la
Kitaifa la wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini litakalofanyika Jijini Arusha linaongozwa
na Kauli mbiu inayosema “Kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini kwa ajili ya kujifunza
na kuboresha Utendaji wa Serikali.”
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.