Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama,
amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazotarajiwa
kunyesha kuanzia mwezi Octoba hadi Disemba mwaka 2023, baada ya Mamlaka ya hali
hewa nchini (TMA) kutoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za msimu wa Vuli
zinazotegemewa kuanza katika kipindi hicho, ambao umeonesha uwepo wa El-NiƱo
itakayosababisha vipindi vya mvua kubwa.
Waziri Mhagama ameyasema hayo ,
alipokuwa akizungumza na waandishi habari katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya
hiyo mtaa wa Posta Jijini Dodoma.
Waziri Mhagama amesema kipindi
hicho cha mvua kubwa kinaweza kuendelea mpaka mwezi Januari 2024, na alisema
kuwa Msimu wa Vuli ni mahususi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa
mwaka unahusisha maeneo ya Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Kusini
mwa mkoa wa Simiyu, Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma, Dar es Salaam, Tanga, Pwani
(ikiwemo visiwa vya Mafia) na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.
“Tunaona madhara kadhaa
yanayoweza kutokea katika baadhi ya sekta kutokana na uwepo huo wa El-nino
utakaosababishwa na mvua kubwa katika kipindi hicho ambacho kimesemwa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini ni kama vile, mafuriko yatakayoleta uharibifu wa
miundombinu, madhara ya kiafya, kiuchumi, kijamii na upotevu wa mali na
maporomoko ya ardhi kuathiri makazi.” Alifafanua Waziri Mhagama
Aidha, aliongeza kusema kuwa
madhara mengine yanaweza kutokea katika Sekta ya mazingira ikiwa ni pamoja na
uharibifu wa mashamba, Miundombinu ya usafiri na shughuli zingine hususani
uchimbaji madini pamoja na magonjwa ya milipuko kwa binadamu, wanyama na
kuongezeka kwa wadudu waharibifu wa mazao na mimea.
Sambamba na hilo, Waziri
Mhagama amesema Serikali inaelekeza kamati za usimamizi wa maafa na sekta,
kushirikiana na umma kuchukua baadhi ya hatua kama vile kutambua maeneo
hatarishi na yenye viashiria vya kuathirika na maafa na kuandaa mipango ya
kuzuia madhara na kukabiliana na maafa endapo yatatokea pamoja na kuainisha na
kuandaa rasilimali za usimamizi wa maafa kwa kila sekta kushiriki kikamilifu
katika eneo lake.
“Tunazielekeza kamati hizo
zisisubiri maafa yatokee, waanze kutambua maeneo yote hatarishi na yenye viashiria
vya kuathirika na maafa na kuanza kuandaa mipango ya kuzuia madhara yoyote
yanayoweza kutoka na utabiri huo wa Mamlaka ya hali ye hewa.” Alisisitiza
Waziri Mhagama
Pia Ameziagiza kamati hizo
kuanza kuandaa na kuainisha rasilimali za usimamizi wa maafa kwa kila sekta kwa
kushiriki kikamilifu katika kuhakikiksha zianaendana na maeneo yao.
Awali Waziri Mhagama
amezikumbusha kamati hizo kuchukua hatua kwa kuzingatia utabiri wa Hali ya Hewa
kwa kuelimisha wananchi kwenye maeneo yao juu ya hatua za tahadhari za kuchukua
ili kuokoa maisha pale ambapo jambo lolote litatokea na kukoa mali na kutoa
taarifa kwa haraka sana kwa mamlaka Husika kuhusu dalili zozote za kutokea
Maafa.
Waziri Mhagama Ametoa wito kwa
wananchi wote wanaoishi na kuendesha shughuli za kiuchumi maeneo ya uwanda wa
chini na pembezoni mwa mabonde ya maji wanatahadharishwa kuchukua hatua ili
kunusuru maisha na mali zao.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.