Wananchi wamepewa wito wa kushiriki
katika wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini itakayofanyika Jijini Arusha
ambayo itahusisha kutoa elimu itakayowawezesha kutoa taarifa za Ufuatiliaji na
Tathmini na Ufuatiliaji wa Miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayofanywa na Serikali
katika maeneo yao.
Hayo yameelezwa leo na Mtakwimu
Mkuu kutoka Idara ya Ufuatliaji na Tathmini ya Ofisi Waziri Mkuu (Sera, Bunge
na Uratibu) Bw. Thomas Saguda, alipokuwa akizungumza na Kituo kimoja cha
Televisheni Jijini Dodoma.
Bwn. Saguda Alisema, Wananchi
hao wanaweza kushirki kupitia maonesho mbalimbali yatakayoonesha kazi mbalimbali
za Ufuatiliaji na Tathmini zilizofanyika ndani ya nchi na kupata kujionea
mengine yatayooneshwa na washiriki mbalimbali kutoka nje ya nchi.
“Maonesho haya yatawapa fursa
wananchi ya kuelewa namna wanavyopaswa kufanya Ufuatiliajia na Tathmini,
wenzetu wataalam wanaita Citizen Science, ni rahisi sana Mwananchi
ukimuuliza mradi flani wa maji pale umefanya kazi, atakwambia unafanya kazi, ama
atakwambia maji pale yalitoka wiki mbili tuu yakakatika, kwa hiyo yule anakupa
taarifa ya uhakika, kwa sababu ndiyo mnufaika na ndiyo mlengwa.” Alisema bwana
Saguda.
Aliendelea kusema kuwa
Sambamba na Maonesho hayo Kongamano hilo pia litahusisha mafunzo ya kitaaluma,
warsha mbalimbali zitakazoendeshwa na wataalamu wabobezi wa masuala ya Ufuatiliajia
na Tathmini kutoka ndani na nje ya nchi na kuongeza kusema kuwa mada mbali
mbali zimekwisha wasilishwa kwa ajili ya Utekelezaji.
Awali akiongea katika kipindi
hicho maalum, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. JohnBosco Quman, alisema Eneo
la Ufuatiliaji na Tathmini linamgusa
kila mmoja, aliyepo Serikalini au katika Sekta Binafsi kwani Utekelezaji wa
Miradi mingi inatekelezeka katika jamii na inamgusa kila mmoja, “Ukiangalia katika
ngazi ya Wizara Sera ndo zinatekelezeka huko, lakini kwenye suala la
utekelezaji linashuka kwenye ngazi ya Halmashauri na ndiko kwenye wadau
mbalimbali, kwa hivyo kwa kupitia miradi kama vile ya Afya na Maji, Serikali
inavyotoa fedha na kusimamia miradi hiyo, matokeo yake yanamgusa kila mmoja.”
Alibainisha Bw. Quman
Aliendelea Kufafanua kuwa
Idara hii ina jumuku kubwa la kuhakikisha kuwa kile ambacho kinachotolewa na Serikali
kinaenda kunufaisha jamii nzima.
Sambamba na hilo, Kongamano
hili la Pili la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini litakalofanyika Jijini
Arusha mapema mwezi Septemba, itawalenga zaidi,wataalam wa Ufuatiliaji na
Tathmini, Maafisa na Mameneja wa Miradi kutoka katika Taasisi zote za Umma, Taasisi
Binafsi, makampuni, Asasi za Kiraia na mashirika ya Kimataifa.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.