Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu nayeshugulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama,
Amepokea Rasimu ya kwanza ya Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya
Utendaji wa Shughuli za Serikali katika Taasisi za Umma.
Akipokea Rasimu hiyo Jijini
Dodoma, Waziri Mhagama alisema Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini
ya Utendaji wa Shughuli za Serikali Nchini, Utasaidia kuwa na matokeo ambayo
yanaendana na programu na Miradi iliyopangwa kutekelezeka ndani ya Taifa, na
Itasaidia Serikali kujipangia Programu zenye matokeo chanya.
“Tunaweza tukawa na matokeo yakawa hasi, ama
mradi usifanye vizuri, ila tukiwa na Mwongozo mzuri basi utatusaidia ndani ta Taifa
kuwa na matokeo mazuri yaliyowekwa kutokana na Utekelezaji wa mradi Husika”
alibainisha.
Sambamba na hilo, alisema
kuwa, mwongozo huu utafikisha Taifa mahali ambapo dhana ya uwajibikaji wa hiari
na uratibu wa Pamoja itafikiwa na kujifanyia tathmini katika usimamizi na
utekelezaji wa programu, zilizopo nchini na Usimamizi mzuri wa Rasilimali watu
na Rasilimali fedha kwenye Serikali kuu, Taasisi na Serikali za Mitaa.
Aidha, Mhe. Waziri Mhagama
Alisema ana Imani kuwa Muongozo huu, utasaidia kuimarisha Utawala Bora na
kuendelea kusema kuwa, bila Utawala bora hakuna kizuri kitakachofanyika, katika
dhana nzima ya kutelekeza kazi za kila siku akitolea mfano dhana ya uwajibikaji
na mapambano dhidi ya rushwa.
“Tunatarajia kuwa Mwongozo huu
Utatusaidia kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo, Ilani ya Uchaguzi ya Chama
Tawala na Mpango wa Maendeleo wa Muda Mrefu na muda Mfupi.” Alihimiza.
Aliongeza kusema kuwa Mwongozo
huu utasaidia kukamilisha programu na miradi Pamoja na kufikisha huduma kwa wananchi kwa wakati na viwango vinavyotarajiwa na
kuokoa Rasilimali fedha kwa kiasi kikubwa.
“Nauona huu Mwongozo ni kitu
cha Muhimu na kipekee,Tunataraji mwongozo huu utusaidie ndani ya Serikali
kupanga miradi na program zetu kwa kuzingatia vipaombele tulivyonavyo, kwenye
Sekta, Taasisi, Mashirika ya Umma na wakala lakini hata kwenye Sekta Binafsi
sababu wale ni washiriki wetu kimaendeleo.” Alifafanua
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kikosi Kazi cha kuandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya
Utendaji wa Shughuli za Serikali Dkt. Fransis Mwaijande, alisema Uandaaji wa
Mwongozo huo umetokana na kuiwezesha Ofisi ya Waziri Mkuu kutekeleza jukumu la
Kikatiba ambapo limeainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungango wa Tanzania
Ibara ya 52 fungu cha 1-3 ya mwaka 1977, mbayo inaipa Ofisi ya Waziri Mkuu
Mamlaka ya Kusimamia Shughuli za Serikali ikiwemo Ufuatiliaji na Tathmini wa
Sera Mipango, Miradi na Programu za Maendeleo na Utendaji wa Shughuli za
Serikali kwa Ujumla.
Awali, Akiongea wakati wa
wasilisho la Mwongozo huo, Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, bunge na Uratibu Bi. Sakina Mwinyimkuu
alisema, rasimu hiyo ya Mwongozo wa Ufuatiliaji na Tathmini ni miongoni mwa document
ambayo itatumika wakati wa kongamano la pili la Kitaifa Ufuatiliaji na Tathmini
litakalofanyika Mwezi Septemba Mkoani Arusha.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.