|
Wataalam wa sekta za
Afya wakijiandaa kumhudumia mgonjwa wa
kuigiza wa Homa ya Bonde la Ufa, aliyeigiza kuwa na ugonjwa huo mpakani mwa Tanzania
na Kenya, kwenye eneo la Namanga wakati wa zoezi
la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 12 Juni, 2019.
|
Na. OWM, Namanga.
Tanzania kwa kushirikiana na Kenya jana tarehe 11
Juni, 2019, wameanza kutekeleza zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, lilofunguliwa
jana mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo
linatekelezwa kwa siku nne, kuanzia
tarehe 11 hadi 14 Juni mwaka huu.
Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja
ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na
mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri
binadamu. Wataalamu wa sekta hizo leo tarehe 12, Juni, 2019, wameendelea
kutekeleza zoezi hilo kwa kuzingatia
Dhana hiyo.
Wataalamu wa sekta za Afya wa Tanzanaia na Kenya, katika
makundi tofauti wameweza kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja
katika kuhakiki matumizi ya maabara
zinazohamishika, kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa
ya Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango
ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza
madhara ya Bonde la Homa ya Ufa kwa
Wanyama na Binadamu.
MWISHO.
|
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee, na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, (Kulia kwake), Waziri Afya wa
Kenya, Mhe. Sicily Kariuki, (Kushoto kwake) Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega wakipata maelezo ya matumizi
ya moja ya maabara inayohamishika, ambayo inatumika katika zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, katika mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo
la Namanga, linalofanyika, hadi
tarehe 14, Juni 2019.
|
|
Timu ya Dharura ngazi ya
Taifa wakipata maelezo kutoka kwa Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Namanga Dkt. Rose Maro, juu ya namna walivyo weza
kuwahudumia wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa, wakati wa igizo la zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mpakani mwa Tanzania na
Kenya, kwenye eneo la Namanga leo tarehe 12 Juni, 2019.
|
|
Timu ya Dharura ngazi ya Taifa wakipata maelezo kutoka kwa Mchinjaji kwenye machinjio ya
Namanga, Athumani Ibrahim, juu ya namna wachinjaji walivyo ugua Homa ya Bonde
la Ufa kwa kuchinja mifugo yenye ugonjwa huo, wakati wa igizo la zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga leo tarehe 12 Juni, 2019 |
|
Mratibu wa Dawati la
Afya Moja Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akifafanua jambo kwa Timu ya
Dharura ngazi ya Taifa wakati wa zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la
Namanga, tarehe 12 Juni, 2019.
|
|
Timu ya Dharura ngazi ya
Taifa wakiwasili katika Kituo cha Afya Namanga, ili kupata maelezo ya namna kituo hicho walivyo weza kuwahudumia
wagonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa, wakati wa igizo la zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mpakani mwa Tanzania na
Kenya, kwenye eneo la Namanga leo tarehe 12 Juni, 2019.
|
|
Wataalam wa sekta za Afya kutoka mashirika ya Kimataifa wakiwa katika chumba maalum cha Menejimenti ya
Taarifa za zoezi la Kupima Utayari wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko
mipakani, leo mpakani mwa
Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, tarehe 12 Juni, 2019.
|
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.