WAZIRI
MKU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu Serikali
itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha
Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blueprint) kwa lengo la
kurahisisha mazingira ya kufanya biashara.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 28) wakati akiahirisha mkutano wa
15 wa Bunge, jijini Dodoma. Amesema wakati kazi hiyo inaendelea
Serikali itafanya ufutialiaji kuhusu utekelezaji wa mpango huo na
kutathmini kama lengo limefikiwa.
”Utekelezaji
wa mpango huo unakwenda sambamba na dhamira ya Serikali ya kurahisisha
mazingira ya kufanya biashara nchini, unaojidhihirisha kupitia sheria ya
fedha ya mwaka 2019 ambayo imefuta tozo kwamishi 54 zilizobainishwa
kwenye mpango huo.”
Waziri
Mkuu ametaja tozo zilizoondolewa au kupunguzwa ni pamoja na
zinazosimamiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula
na Dawa (TFDA), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),
Wizara ya Mifugo na Uvuvi hususan kwenye Sekta ya Mifugo, Wizara ya
Maliasili na Utalii na Wizara ya Maji
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo
unaleta tija, ameielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara ishirikiane na
Ofisi ya Waziri Mkuu kusambaza blueprint pamoja na Mpango Kazi wa
Utekelezaji kwa wizara zote kwa ajili ya kusimamia utekelezaji katika
maeneo yao.
Amesema
kupitia mpango wa bajeti ya 2019/2020, Serikali itaendelea kuweka
mazingira rahisi ya ufanyaji biashara kwa kutoa unafuu katika sekta za
kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli nyingine jumuishi.
Wakati huohuo,Waziri
Mkuu amesema katika kukabiliana na kilimo tegemezi cha mvua hususani
kwenye zama hizi za mabadiliko ya tabia nchi, Serikali kwa sasa
inaboresha kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kuwatoa wananchi katika
kilimo hicho.
Amesema
hatua zilizochukuliwa hadi sasa ni pamoja na kuunda upya Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji ambayo inalenga kuiwezesha tume hiyo kusimamia ipasavyo
shughuli za umwagiliaji. Pia Serikali imehamishia tume hiyo Wizara ya
Kilimo ambayo ndiyo yenye dhamana ya kuendeleza kilimo nchini.
”Ili
tuweze kufikia lengo la kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka
hekta 475,056 za sasa hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2025, tayari
nimeielekeza Wizara ya Kilimo isimamia kwa karibu na kutekeleza majukumu
yake kwa weledi.”
Waziri
Mkuu amesema Wizara ya Kilimo inatakiwa ihakikishe inasimamia vema
miradi 22 ya umwagiliaji inayoendelea sasa pamoja na miradi mipya minane
itakayojengwa nchini katika pindi cha mwaka wa fedha 2019/2020.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.