WAZIRI
MKU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta
binafsi katika kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji na
biashara.
Amesema
mpaka sasa, hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa kwa lengo la
kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini.
Ameyasema
hayo leo (Alhamisi, Juni 27, 2019) jijini Dodoma wakati akifungua
kongamano la uwekezaji la mkoa wa Dodoma kwa niaba ya Rais Dkt. John
Magufuli.
”Miongoni mwa hatua hizo ni uwepo wa usafiri wa uhakika na wa haraka wa abiria na mizigo kwa kujenga reli ya kiwango cha kimataifa (Standard GaugeRailway).”
Pia, Waziri Mkuu amesema uwanja wa ndege wa Dodoma umeboreshwa na kuruhusu ndege kubwa na ndogo kutua usiku na mchana.
”Mashirika
ya ndege yanayotoa huduma yameongezeka na maandalizi ya awali ya ujenzi
wa uwanja wa kimataifa wa ndege katika eneo la Msalato yanaendelea.”
Waziri
Mkuu amesema mkoa wa Dodoma una barabara za kuaminika za kiwango cha
lami zinazoiunganisha na mikoa mingine pamoja na nchi jirani.
Amesema
Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuboresha huduma za afya na Dodoma
kuna hospitali ya Benjamin Mkapa yenye uwezo kama wa Muhimbili na
Mloganzila.
Amesema ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji ‘Stiegler’s Gorge’wenye uwezo wa kuzalisha MW 2,115, utaongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika nchini.
“Mradi
huo utaongeza upatikanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika kwa ajili
ya kukidhi mahitaji ya viwanda na uwekezaji nchini ikiwemo na katika
mkoa wa Dodoma.
Waziri
Mkuu amesema Serikali itaendelea na utekelezaji wa mpango wa Kuboresha
Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (The Blue Print) utakaoanza Julai
mosi mwaka huu.
Waziri
Mkuu amesema anatarajia kuwa kongamano hilo litawezesha kupatikana kwa
wawekezaji mahiri kwa maendeleo ya uchumi na wananchi wa Tanzania.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge alisema katika azma ya
Selikali ya kujenga uchumi wa viwanda wameandaa kongamano hilo ili
kutangaza fursa zilizopo.
Alisema
kaulimbiu ya kongamano hilo ni ‘Dodoma Fursa Mpya Kiuchumi Tanzania,
Wekeza Dodoma Tukufanikishe’, inatanabaisha nafasi ya mkoa huo kwa sasa
na baadaye.
Dkt.
Mahenge alitaja baadhi ya fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Dodoma
kuwa ni pamoja na uwepo wa ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo, viwanda
na taasisi (afya, elimu).
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.