Na.
OWM, ARUSHA
Wataalam wa maabara nchini kwa kutumia Dhana
ya Afya moja ambao ni wataalam wa
maabara kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja
na mazingira wameendelea kupewa mafunzo ya Msingi ya Usimamizi na udhibiti wa vimelea hatarishi vya kibailojia kwa kuimarisha ulinzi na
usalama wa sampuli za vimelea hivyo.
Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa
wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa
kuvichukua kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa
kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya
Uchunguzi pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu
mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, leo
tarehe 29, Julai, 2019, Mratibu wa Afya
Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amefafanua kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo
ya msingi ambayo wataalam hao tayari walishafundishwa mafunzo ya awali ya
Usimamizi na Usalama wa vimelea
hatarishi vya kibailojia mnamo mwezi Machi, mwaka huu.
“Lengo la mafunzo haya ni kuiwezesha nchi yetu
kuwa na wataalamu wa maabara wenye uelewa kuhusu dhana ya vihatarishi vya
kibaiolojia, kuandaa na kusafirisha sampuli za vimelea kwa usahihi na pamoja na ulinzi na usalama wa
vimelea” amesema Chinyuka
Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa
mafunzo hayo wamebainisha kuwa baada
ya mfunzo hayo, mienendo na matendo yao wakiwa maabara itazingatia usalama wa afya zao na usalama
wa jamii inayowazunguka pamoja na Usalama wa watanzania, kwa kusimamia na
kudhibiti vihatarishi vya kiulinzi na
usalama vitokanavyo na vimelea hatarishi amabavyo wataalamu hao wamepewa
dhamana ya kuvifanyia kazi.
Mafunzo
hayo ya siku tano, yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Defence Threat Reduction Agency -DTRA na
Sandia National Laboratories na
wawezeshaji wa hapa nchini kutoka wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia ,
Wazee na watoto pamoja na Wizara ya Uvuvi na Mifugo.
Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na
mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri
binadamu ,wanyamapori na mifugo.
MWISHO.
Mshiriki wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya
kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, Fredy
Makoga, akichangia wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
|
Mshiriki wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya
kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, Basilius
Kilowoko, akichangia wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
|
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.