*Wazungumzia namna ya kuimairisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana
na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah Al- Sisi, ambapo
wametumia fursa hiyo kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna ya
kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Misri.
Mbali
na kuzungumzia masuala hayo ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja
mbalimbali zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kijamii, pia Waziri Mkuu
amemfikishia Rais wa Misri salamu kutoka kwa Rais wa Tanzania Dkt. John
Magufuli.
Mazungumzo
baina ya Waziri Mkuu na Rais wa Misri yamefanyika leo (Jumatano, Juni
10, 2019) Ikulu jiji Cairo, ikiwa ni katika siku ya tatu na ya mwisho ya
ziara yake ya kikazi nchini Misri. Katika ziara hiyo ameambatana na
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.
Waziri
Mkuu amemaliza ziara yake ya kikazi nchini Misri ambapo katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Cairo ameagwa na Waziri wa Kilimo na
Uhaulishaji wa Ardhi wa Misri, Dkt. Ezz Eldien Abo Setit.
Akiwa ziarani nchini Misri, Waziri Mkuu alikutana
na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly
katika siku yake ya kwanza ya ziara yake, ambapo aliwakaribisha
wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.
Pia,
Waziri Mkuu alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo
ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa makao makuu mapya ya nchi hiyo,
mradi wa awamu ya pili ya upanuzi wa mfereji wa Suez Canal na kiwanda
kikubwa cha ngozi.
(mwisho)
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.