*Waziri
Mkuu asema hadi Julai 30 wakulima wote watakuwa wamelipwa
Na Mwandishi Wetu
ZAO la pamba ni miongoni mwa mazao makuu ya biashara hapa nchini yakiwemo
ya korosho, chai, tumbaku, katani na chikichi ambayo yamekuwa yakitegemewa
katika kuinua uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Hivi karibuni kumetokea hali ya sintofahamu kuhusiana na suala ununuzi
wa zao hilo baada ya kutangazwa kwa bei elekezi ambayo ni sh. 1,200 kwa kilo moja
katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.
Bei elekezi ya pamba kwa msimu huu ilitangazwa Aprili 30, 2019 mkoani Shinyanga na kwamba bei hiyo ilitakiwa ianze kutumika kuanzia Mei 2, 2019. Hata hivyo ununuzi wa zao hilo ulianza kwa suasua jambo ambalo Serikali haikuridhishwa nalo.
Jumapili ya Julai 14, mwaka huu ndipo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliamua
kuitisha kikao kilichojumuisha wakuu wa mikoa 11 inayolima pamba, wanunuzi wa
zao hilo, taasisi mbalimbali za kifedha pamoja na Gavana wa Benki Kuu.
Kikao hicho kilichoitishwa na Waziri Mkuu na kufanyika katika ukumbi wa
Mtemi Isike Mwanakiyungi kilikuwa na lengo la kutafakari mwenendo wa zao la
pamba ambalo ununuzi wake unaendelea lakini kwa kasi ndogo.
Waziri Mkuu baada ya kusikiliza changamoto za wanunuzi ambao wengi wao
waliomba Serikali iwadhamini katika taasisi mbalimbali za fedha walizoomba
mikopo kwa ajili ya kununua zao hilo kwa kuwa ilikuwa imekwama. Serikali iliwakubalia.
“Sasa tumefikia muafaka wa jambo hili kibali kitatoka na wote
watakaopata dhamana ya mikopo hakikisheni fedha hizo zinaenda kutumia kwa ajili
ya ununuzi wa pamba kama ilivyokusudiwa na si vininevyo.”
Hivyo,
Waziri Mkuu aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya katika maeneo yote yanayolima
pamba wawasimamie ipasavyo wanunuzi wote ili kuhakikisha fedha zitakazopatikana
zinakwenda kutumika kwa ajili ya kununulia pamba.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi Binafsi wa Pamba (TCA), Bw.
Christopher Gachuma aliishukuru Serikali kwa kukubali kuwadhamini pamoja na
Waziri Mkuu kwa maelekezo aliyoyatoa kuhusu suala la ununuzi wa zao hilo.
Waziri Mkuu, baada ya kufanya kikao na wadau wa pamba wakiwemo na wanunuzi ambao walikubali kwenda kununua pamba iliyoko kwa wakulima, Julai 15, 2019 alifanya ziara katika wilaya ya Igunga kwa lengo la kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Akiwa
katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alianza kwa kukagua ghala la ununuzi wa pamba la
AMCOS ya Mbutu na kisha alikwenda katika kijiji cha Mwabakina na kukagua ghala
la kununulia pamba la Mwabakima.
Baada ya
kukagua maghala hayo Waziri Mkuu alizungumza na wananchi wa maeneo hayo ambao
wengi wao ni wakulima wa pamba ambapo aliwahakikishia kwamba hadi kufikia
tarehe 30 mwezi Julai mwaka huu pamba yote iliyoko katika mikoa mbalimbali
nchini itakuwa imeshanunuliwa na wakulima wote kulipwa fedha zao.
Alisema
Serikali imeamua kuingilia kati suala la ununuzi wa zao la pamba kutokana na
kusuasua kwa soko lake kwa kutoa dhamana ili kuwawezesha wanunuzi kukopeshwa
fedha na benki mbalimbali kwa ajili ya kununulia pamba kutoka kwa wakulima.
“Tunatambua
adha mliyoipata tangu kuanza kwa msimu wa mwaka huu na hayo ni mapito tu.
Nawasihi muwe na amani kwani Serikali yenu inafuatilia suala hili na Rais Dkt.
John Magufuli anataka kuona pamba yote inatoka kwa wakulima ili kuwawezesha
kupata tija.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwasihi wakulima wa zao hilo la pamba na wakulima wa mazao
mengine nchini wahakikishe mara baada ya kuuza mazao yao wanatenga kiasi cha
fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo watakazozitumia katika msimu ujao.
Wananchi
kwa upande wao waliishukuru Serikali kwa hatua yake ya kuingilia kati suala la
ununuzi wa zao la pamba pamoja na malipo kwa wakulima ambao tayari pamba yao
walishaipeleka katika AMCOS zao.
Kwa upande
wake, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga
alisema Serikali itahakikisha inaendelea kutafuta masoko ya mazao hayo ndani na
nje ya nchi ili kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa masoko kwa mazao yao na
hivyo kujiongezea tija.
Pia,
Waziri huyo alisema mbali na kutafuta masoko, Serikali imedhamiria kufufua
viwanda mbalimbali vya nguo hapa nchini ili kuwawezesha wakulima wa zao la
pamba kuwa na soko la uhakika. “Kuhusu suala la maghala tunatambua tatizo hilo
na tutahakikisha tunayaboresha ili pamba iweze kuhifadhiwa katika mazingira
bora”.
Akizungumzia
kuhusu changamoto ya viuatilifu, Waziri Hasunga alisema Serikali itahakikisha
vinapatikana kwa kuzingatia eneo husika ili kuweza kudhibiti wadudu waharibufu.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.