Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewashukuru wadau mbalimbali
wanaoendelea kujitolea na kutoa michango kwa ajili ya maafa ya Kuporomoka kwa
ghorofa eneo la Kariakoo kusema ni moyo wa upendo unaoneshwa kwa matendo
mbalimbali walioguswa na maafa hayo.
Ametoa shukrani hizo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu hatua
zinavyoendelea katika eneo lililopatwa na ajali ya kuporomoko kwa jengo la
ghorofa mtaa wa Agrey Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Yonazi ametumia nafasi
hiyo kutangaza “Control Number” kwa ajili ya kuwawezesha wananchi ambao
wataguswa na maafa hayo kwa kutuma michango yao kwa ajili ya kuendelea kusaidia
katika hatua baada ya kutokea maafa hayo.
" Control number ni
987320001709 ambapo namba hii inatumika kwa mitandao yote ,mwananchi anaweza
kuchangia kuanzia 1000 na kuendelea na fedha hizi zinaingia moja kwa moja
kwenye akaunti ya Maafa au kuchangia kupitia akaunti ya National Relief Fund
yenye namba 9921159801 ambayo ipo Benki Kuu ya Tanzania,” amesema Dkt.Yonazi.
Kwa hatua nyingine Dkt. Yonazi
amepokea msaada kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
lililokabidhi kiasi cha shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini kwa lengo la
kusaidia kufuatia maafa hayo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
hundi hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Jenerali mstaafu George
Waitara amesema kuwa tukio hilo limesababisha maafa makubwa ikiwemo
vifo,uharibifu wa mali pamoja na matatizo ya kisaikolojia kwa waathirika wa
tukio hilo.
"TANAPA ni sehemu ya
wananchi wa Tanzania,hivyo janga hili tumetugusa tukaona tutoe chochote
kusaidia uokoaji wa maafa haya na Watanzania wasiwe na taharuki kwani tumeona
shughuli za uokoaji zinakwenda vizuri, kikubwa wawe wanafuatilia taarifa
kupitia mamlaka husika na si vyanzo vingine " amesema Jenerali Mstaafu
Waitara.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.