Ujumbe kutoka Mfuko wa
Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ukiwa umeambatana na watumishi wa
Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
pamoja na watekelezaji wa programu hiyo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi
ya Rais, TAMISEMI, Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi Zanzibar wamekitembelea Kikundi cha Ufugaji wa samaki
kiitwacho UWASAMO, katika kata ya Mzinga Mtaa wa Konga Manispaa ya Morogoro,
ili kuona mafanikio ya ufugajiwa samaki kwa wanakikundi baada ya kupata mafunzo
ya Ufugaji samaki, biashara na utunzaji wa kumbukumbu kutoka kituo cha Kingolwira.
Ziara hiyo imefanyika leo
tarehe 6/11/2024 kwenye Kituo kinachojishughulisha na utoaji mafunzo ya ufugaji
samaki, pamoja na uuzaji wa vifaranga vya samaki.
Akizungumza kwa niaba ya
wanakikundi ndugu Asungushe Patrick Msugupakulya amesema, wao kama kikundi
wanaishukuru serika kwa kuwaletea mradi wa IFAD, ambao umewasaidia katika kuunda
ushirika wao ambao mpaka sasa wanaendelea kupata msaada wa Elimu ya ufugaji wa
samaki kwa wakati.
Pamoja na hayo wanakikundi cha
UWASAMO, wamefurahishwa na ziara ya viongozi, ambapo wanaamini kwa kutembelewa
huko, misaada zaidi watapata ili kuendeleza mtaji wao wa ufugaji wa samaki na
kuleta maendeleo yenye tija kwa familia na Tanzania kwa ujumla wake.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.